VIDEO Queen, Agnes Jerald ‘Masogange’ hivi karibuni alibambwa maeneo ya Sinza Kamanyola jijini Dar akijiachia na anayetajwa kuwa ni mpenzi wa Jack Patrick, Juma Khalid ‘Jux’.
Masogange akipozi na Jux.
Wawili hao walibambwa kwenye duka moja lililopo maeneo hayo baada ya
Jux kutua kutoka China huku Agnes akionekana kama anayemfariji kwa tukio
la Jack kunaswa na madawa ya kulevya.
Jux akiwa na mpenzi wake Jack Patrick.
Akiuzungumzia ukaribu wake na Jux, Masogange alisema: “Wala hakuna
lolote kati yangu na yeye. Mimi na wale akina Jux pamoja na dada yake ni
watu wangu wa karibu sana tunaojuana muda mrefu hivyo tulikuwa
tunabadilishana mawazo tu.”
Masogange akiwa na Jack.
Jux na Jack wamekuwa wakionekana katika mitaa ya China wakila bata
huku kukiwa na madai kuwa ni wapenzi na kuonekana kwa Jux na Masogange
wakijiachia kumeibua maswali mengi.