Jitihada za kuuzima moto huo zilivyokuwa |
BWENI la wavulana wa shule ya sekondari Njombe mkoani Njombe
limeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Njombe, Fulgency Ngonyani amesema moto huo ulisababishwa na hitilafu
ya umeme iliyotokea katika bweni hilo.
Alisema bweni hilo lilikuwa likitumiwa na wanafunzi 42 wa
kidato cha tano na sita.
Alizitaja baadhi ya mali zilizotekea kwa moto huo kuwa ni pamoja na vitanda, magodoro, mabegi ya nguo na nguo zilizokuwemo, masunduku ya vitabu na fedha taslimu.
Pamoja na kuteketeza mali hizo, moto huo
haukumdhuru mwanafunzi hata mmoja kwani ulipoanza kuwaka wengi wao hawakuwepo
bwenini.
Uongozi wa shule hiyome umekadiri hasa
iliyotokana na moto huo kuwa zaidi ya Sh Milioni 63.