MALI ZA NELSON MANDELA ZATANGAZWA HADHARANI

Marehemu Nelson Mandela enzi za uhai wake.
MALI za marehemu Nelson Mandela, zimetangazwa ambapo aliiachia familia yake mali za dola milioni 4.1 sawa na bilioni 6.7 za Tanzania.
Sehemu ya mali hiyo itatolewa kwa chama tawala cha ANC, wafanyakazi wake wa zamani na shule kadhaa ambako alisomea.
Mali hizo zinajumuisha nyumba na hakimiliki za vitabu kikiwemo kimoja kuhusu maisha yake kiitwacho ''Long walk to freedom''.
Hayo ndio yalikuwa mapenzi ya Mandela ambayo yalikuwa kwenye wosia wake uliosomwa hadharani kwa familia nzima.
Ofisa Dikgang Moseneke aliyekabidhiwa jukumu la kusoma wosia huo wenye kurasa 40 na kuhakikisha unatekelezwa, alisema hapajakuwa na pingamizi lolote kuhusu yaliyomo kutoka kwa familia ya Mandela.
Wafanyakazi wa karibu wa Mandela watapata randi 50,000 kila mmoja. Shule ambazo Mandela alisomea zitapata randi 100,000 kila shule.
Hayati Mandela alifariki Desemba 5, 2013 akiwa na umri wa miaka 95.
Familia ya Mandela tangu hapo imekuwa ikizozana kuhusu urithi wa hayati Mandela na kuna hofu kuwa huenda wosia huu ukasababisha mgogoro mwingine kuhusu mali hiyo


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...