Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Affani Othman Maalim (kulia) kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akitiliana saini makubaliano ya uanzishwaji wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa Wanawake na Chuo cha Barefoot cha India ambapo muanzilishi wa Chuo hicho Bw. Bunker Roy alitia saini (kulia). Saini hiyo ilifanyika wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika ziara rasmi nchini India na ujumbe wake.
Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo na Maliasili Affani Othman Maalim (kulia) akibadilishana hati za
makubaliano na Bw. Bunker Roy baada ya kutiliana saini makubaliano ya
uanzishwaji wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa Wanawake baina ya Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar na Chuo cha Barefoot cha India, saini hiyo
ilifanyika wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika ziara rasmi nchini India na ujumbe
wake.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akibadilishana
mawazo na Bw. Bunker Roy Muanzilishi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa
Wanawake katika Kijiji cha Tilonia Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan
pamoja na Balozi wa India nchini Tanzania Debnath Shaw (kulia) baada ya
saini ya makubaliano ya uanzishwaji wa chuo kama hicho Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Bw. Bunker Roy.
[Picha na Ramadhan Othamn, Ikulu]