Muigizaji
wa kike wa filamu za kiswahili, Wastara Juma amesema tangu mme wake
Juma Kilowoko aka Sajuki afariki anakutana na changamoto nyingi kwenye
mazingira yaliyomzunguka kwa sasa.
Akizungumza
na tovuti ya Times FM 100.5, Wastara amesema tangu Sajuki afariki
kumekuwa na taarifa zisizo za kweli zinazodai kwamba amepata mume.
“Nina changamoto nyingi
sana,unajua siku zote kama mtu ukitaka kuheshimiwa basi heshima ndio
msingi wa maisha,lakini tangu mume wangu afariki (Sajuki)kumekuwa na
maneno mengi sana kwenye magazeti,mara nimeolewa sijui nimevishwa pete
na ukija kuangalia mtu aliyeandikia hiyo habari unamjua na ukimpigia
simu anaanza kukukwepa. Kama habari za kuolewa siwezi kwanza kutangaza,
naomba waandishi waandike habari za uhakika ili ujumbe ufike mzuri kwa
wananchi wanaotutazama sisi Wasanii.” Amesema Wastara.
Katika hatua nyingine Wastara
amesema mwaka huu amejipanga vizuri katika kutoa filamu zake mpya
sinazotarajia kutoka hivi karibuni.
“Mwaka jana mwishoni
nilijikita sana kwenye kuandaa filamu mpya za kwangu na nyingine
nimeshiriki kwa hiyo mashabiki wakae tayari.”
CREDIT : TIMES FM WEBSITE