KULEA KUMEMKOSESHA DILI SUPER STAR BONGO MOVIE DAVINA

Na Gladness Mallya
STAA wa Bongo Movie, Halima Yahaya ‘Davina’ amefunguka kuwa mwaka 2013 aliutumia zaidi kwa kulea mimba hadi kujifungua hivyo kukosa madili ya kazi za uigizaji.
Halima Yahaya ‘Davina’.
Akizungumza na paparazi wetu, Davina alisema mwaka huu amejipanga kurejea upya katika sanaa kwani amegundua kuwa mashabiki wake walikuwa wamemmisi hivyo lazima apambane kutetea taito yake katika sanaa.
“Nimejipanga zaidi mwaka huu, nimedhamiria kufanya mapinduzi makubwa katika sanaa tofauti na kipindi cha nyuma, kulea siyo mchezo ilibidi sanaa ikae pembeni kidogo,” alisema Davina ambaye sasa ni mama wa mtoto mmoja, Fazal.

GPL


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...