WAZIRI MKUU WA CCM ATAKA CHAMA CHA MAPINDUZI KUMKARIPIA EDWARD NGOYAI LOWASSA

Mzee malecela akionesha moja ya vionjo vya safari



Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na niwapongeze kwa kufika  mwaka mpya 2014,pia naomba niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la TanzaniaNdugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM),kilichonisukuma zaidi na kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia  na kumuona kijana wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana paul makonda akiwa na ujasiri wa kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhi ya viongozi bila uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.Nadiriki kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za kijasiri kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee kupendwa na kuchaguliwa na watanzania.
Pia itakuwa si busara kama sitawapongeza vijana wangu katibu mkuu wa chama ndugu ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi zao za dhati za kujenga chama na kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya chama cha mapinduzi (CCM)kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali cheo na umaarufu wao ndani ya chama na serikali,nawaomba waendelee  na juhudi zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watru wanaowabeza naomba wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya chama na serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda serikali.

 Aidha nawaomba watanzania wenzangu wazalendo wasikubali kukatishwa tama na kikundi cha watu wachache wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo limekuwa mfano wa kuigwa kwa amani,upendo,utulivu na mshikamano urithi tulioachiwa na baba yetu wa taifa mwalimu julias kambarage nyerere ndani na nje ya mipaka ya bara letu la afrika.

Ndugu zangu waandishi wa habari naomba niwaambie kuwa msemaji wa UVCCM kijana wetu paul makonda namuunga mkono kwa  kitendo chake cha ujasiri cha kumkemea ndugu EDWARD NGOYAI LOWASA bila uwoga kwa jinsi anavyokivuruga chama chetu kwa lengo la kutaka urais 2015 huku secretariet ya chama ikiwa imekaa kimya wakati inajua kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi na katiba  ya chama.hapa najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani ya chama chetu cha mapinduzi iko wapi?mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya?je!hapa chama kiko wapi?

Mzee malecela akizungumza leo mchana
Ukweli ni kwamba wanachama wetu na vijana wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia tamko au karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais 2015 bila mafanikio.

Naomba niseme kuwa bila kuwa na karipio au tamko la chama, hawa wanaotumia pesa zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama.

Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu ABDULRAHMANI KINANA na katibu mwenezi NAPE NNAUYE za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga.

Ninaomba juhudi hizi zisibezwe na watu wenye nia njema na chama.,ukweli ni kwamba vijana hawa wamekuwa na juhudi kubwa sana ya kujenga na kuimarisha chama chetu  kwa wananchi kila pembe ya taifa letu kwa kukemea na kueleza misingi ya uongozi bora. swali:je! Chama hakioni haya mpaka vijana ndio waone?

Kwa hili ni lazima tubadilike ili kujenga chama chetu na naishauri  secretariet ya chama lazima ichukue hatua mara moja,kijana huyu paul makonda asingesema haya yote kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya aliyoyasema na nampongeza sana.
Mzee malecela akionesha moja ya vionjo vya safari
Vijana na wanachama wengi wa CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya kutaka kujua msimamo wa chama chao bila mafanikio na ndio sababu ya baadhi ya
 wengine kupoteza mwelekeo.

Sisi tulikijenga chama hiki kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka.nidhamu,busara na uchungu wa rasilimali za taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndio vilituongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na serikali,ndio maana tunaumia sana kuona chama sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka,mpaka tunashangaa na kujiuliza hizi pesa wanatoa wapi?na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa maslahi ya nani?huku watanzania wakiendelea kuwa maskini.

Mfano hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana kwenye vyombo vya habari,vitendo hivi havina tija kwa chama na wala havileti umoja na mshikamano ambao umedumu ndani chama kwa muda mrefu.

Mwisho Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu makonda na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi kwamba utaleta kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima.


MWISHO

JOHN SAMWELI MALECELA

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...