WANAFUNZI
wa chuo cha ualimu Kleruu kilichopo Gangilonga mjini Iringa, wamefanya
maandamano wakipinga kukosa huduma ya umeme kwa wiki ya tatu sasa baada
ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuwakatia.
Maandamano hayo yaliyoanzia chuoni hapo jana kuelekea ofisini na hatimaye
nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa,
yalidhibitiwa na Jeshi la Polisi yakiwa yamekaribi shule ya msingi
Um-salam kwa kile kilichoelezwa kwamba hayakuwa na kibali..
Rais wa serikali ya wanafunzi ya chuo
hicho, Manfred Joachim alisema wametii amri ya Polisi lakini watayafanya
tena Jumatatu baada ya kukamilisha taratibu zote ikiwa ni pamoja na
kupata kibali cha Polisi.
Joachim alisema wameamua kutumia mbinu hiyo ili kuongeza msukomo kwa uongozi wa chuo na serikali kuitatua kero hiyo.
“Hatuwezi tena kujisomea usiku na
mafunzo ya teknlojia ya habari na mawasiliani yaani ICT yamesimama;
wanafunzi wamekata tamaa, hawajui hatma yao wakati ada wamelipa,”
alisema.
Wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa
michezo wa chuo hicho chini ya ulinzi wa Polisi, kiongozi huyo alisema
huduma ya maji nayo ni kero kubwa chuoni hapo.
“Wakati mwingine zinaweza kupita zaidi
ya siku mbili hatujaoga; yote hayo ni kwasababu tuaambiwa na uongozi wa
chuo kwamba hawana fedha za kulipia huduma hizo,” alisema.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Anjelist
Mlenga alisema uongozi wa chuo unawaonea huruma wanafunzi hao lakini
akakosoa taratibu wanazozitumia kudai huduma hizo.
Akiwa hajui kiasi cha fedha kinachodaiwa
kwa ajili ya huduma ya maji, Mlenga alisema deni la umeme chuoni hapo
ni zaidi ya Sh Milioni 2.5.
Alisema Mkuu wa chuo hicho amekwenda wizarani kufuatilia fedha hizo kwakuwa wao ndio wenye jukumu la kulipia huduma hizo.
“Mkuu wa Chuo yupo wizarani, naomba muwe
wavumilivu kwani hata kama atakubaliwa fedha hizo, kwa taratibu za
serikali inaweza kuchukua wiki nyingine kuzipata,” alisema.
Akizungumzia ombi la wanafunzi hao la
kukifunga chuo hicho mpaka pale huduma hizo zitakaporejea, Mlenga
alisema “ ni jambo linalojadirika, tutaona mpaka wiki ijayo hali
itakavyokuwa na tutaangalia cha kufanya.”
Aliwasihi wanafunzi hao kuacha
kuyachanga madai yao na itikadi zao za kisiasa kwa kuzingatia kwamba
mambo hayo yanapigwa marufuku katika taasisi za elimu.
Wanafunzi hao wakiwa na mabango mbali mbali leo katika viwanja vya chuo hicho
Polisi wakithibiti maandamano hayo
WAnafunzi hao wakiwa katika viwanja vya chuo hicho leo
Makamu Mkuu wa Chuo, Mlenge
Rais wa serikali ya wanafunzi, Manfred Joachim
Makamu Mkuu wa Chuo, Mlenge
Rais wa serikali ya wanafunzi, Manfred Joachim
cretid -Habari vyuoni