Lori la mafuta baada ya kuteketea kwa moto kijiji cha Fulwe, wilayani Mikese mkoani Morogoro.
Lori la mafuta na semitrela vikiteketea kwa moto baada ya ajali.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto wakijaribu kutuliza moto huo.
Zoezi la kuzima moto na kusafisha barabara likiendelea.
Semitrela lenye namba za usajili T 499 AUD baada ya ajali hiyo.
Gari la Kikosi cha Zimamoto likiwa eneo la ajali.
Kijiji cha Fulwe ilipotokea ajali hiyo.
AJALI hii imetokea leo katika kijiji cha Fulwe, kata ya Mikese mkoani
Morogoro ambapo malori mawili yamegongana na kuteketea kwa moto.Katika ajali hiyo, dereva wa lori moja lililokuwa na shehena ya mafuta amepoteza maisha wakati dereva wa lori lingine aina ya semitrela akijeruhiwa pamoja na tingo wake na kukimbizwa hospitali.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo amedai kuwa dereva aliyepoteza maisha alishindwa kujiokoa baada ya ajali kutokea kwa kubanwa hali iliyopelekea kuungua vibaya kwa moto.
"Lori hili la mafuta lilikuwa likitoka Dar na kushuka mteremeko huu kwa kasi huku semitrela likijaribu kulipita lori lingine eneo hili hivyo kugongana uso kwa na lori la mafuta.
Baada ya kugongana, mafuta yaliokuwa kwenye tenki yalimwagika hali iliyosababisha malori yote kuteketea kwa moto. " Alisema shuhuda huyo mkazi wa kijiji cha Fulwe, Bw Issa Athuman.
(PICHA ZOTE NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL)