Muimbaji wa ‘Nimevurugwa’ Snura amesema tangu video yake ya ‘Nimevurugwa’ ifungiwe kuchezwa kwenye TV na iondolewe kwenye mchakato wa tuzo za KTMA 2014, amejirekebisha kwa kiasi kikubwa.
“Tayari
mimi nimeshabadilika kabla hata hatujafika huku kwenye Kili, sababu
ilifungikiwa muda kidogo kabla mambo ya Kili hayajaingia na wimbo wangu
wa ‘Ushaharibu’ nilikuwa nimeshafanya video pia, kwahiyo ukitoka watu
watajua ni jinsi gani nimeweza kubadilika,” Snura amekiambia kipindi cha Mitikisiko ya Pwani cha Times FM Alhamis hii.
“Wakati
nafanya video ya Nimevurugwa sikuhisi kama ningefungiwa na kama
ningejua naweza kufungiwa nisingekatika. Kitendo cha mimi kufungiwa
kimenishtua kidogo na nisingependa niende tofauti na BASATA ningependa
niende nao sawa, kwahiyo nilichokifanya kwenye wimbo wangu wa
Ushaharibu, nimekatika ndio lakini hakuna viuno kama ambavyo vipo kwenye
Nimevurugwa.”
Snura
amewaomba radhi mashabiki wake wanaopenda viuno kuwa katika video zake
zijazo hawataviona kama kwenye video zilizopita lakini wataendelea
kuviona akitumbuiza jukwaani. “Na hii nafanya kwasababu tu natafuta riziki si kwamba nafanya hivi labda napenda sana kuonesha kiuno changu stejini,” alisema na kuongeza kuwa mashabiki wake huchukia pale anapotumbuiza bila kuwapa viuno.
“Mimi
ni mfanyabiashara, sina jinsi inabidi nimridhishe mteja wangu ili
waweze kujaa kwenye show, ili waweze kunikubali nipate riziki, mimi
natafuta riziki.”