EL CLASICO: LIONEL MESSI APELEKA VILIO KWA WAPENZI WA REAL MADRID BAADA YA KUTUPIA 'HAT-TRICK'

Lionel Messi (kushoto) akishangilia bao lake la tatu na wachezaji wenzake Gerard Pique (katikati) na Alexis Sanchez.
Karim Benzema akishangilia na wachezaji wenzake wa Madrid Angel Di Maria na Marcelo baada ya kufunga bao la pili.
Iniesta baada ya kufunga bao la kwanza akipongezwa na Jordi Alba (kushoto) na Dani Alves (katikati). Pembeni ni Neymar na Messi.
Pepe juu akishangilia pamoja na wenzake wa Madrid baada ya bao la tatu lililofungwa na Ronaldo.
Mashabiki wa Real Madrid na mabango yao.
Inakuwaje! Pepe akimshika tai Fabregas wakati wa mtanange huo. Pembeni ni Neymar.
Sergio Ramos akionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Neymar.
MSHAMBULIAJI mahiri wa Barcelona, Lionel Messi, usiku huu amepeleka vilio kwa mashabiki na wapenzi wa Real Madrid baada ya kufunga 'hat-trick' wakati timu yake ikishinda bao 4-3 dhidi ya mahasimu wao Real Madrid.
Mechi hiyo kali ya La Liga imechezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabéu, Madrid nchini Hispania.
Mshambuliaji huyo amefunga mabao mawili kwa penalti dakika ya 65 na 84 wakati lingine akilifunga dakika ya 42 baada ya Andres Iniesta kufunga mapema dakika ya 7.

Mabao ya Madrid yamewekwa kimiani na Karim Benzema aliyetupia mawili dakika ya 20 na 24 la tatu likifungwa na Mchezaji Bora wa Dunia mwaka 2013/14, Cristiano Ronaldo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 55.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...