Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi
wa kijiji cha Mkenge kata ya Fukayose Jimbo la Chalinze jana.
Mwenyekiti
wa kata ya Fukayose, Orinjulie Machanga akiwahutubia wananchi wa kijiji
cha Mkenge wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea Ubunge wa Jimbo la
Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete.
Baadhi
ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa wameshikilia picha za
mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Bw. Ridhiwani
Kikwete katika mkutano wa kampeni kijiji cha Mkenge.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na
wananchi wa kijiji cha Mkenge mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa
kampeni kijijini hapo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze, Bw. Ridhiwani Kikwete akihani msiba katika moja ya kijiji kwenye kata ya Fukayose.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na
wananchi baada ya kuwasili katika kata ya Fukayose Jimbo la Chalinze
wakati alipoendelea na mikutano ya kampeni kuwania kiti cha ubunge jimbo
la kata hilo. Ridhiwani Kikwete amewaomba wananchi wa kata ya Fukayose
kumuamini na kumpa kura za ndiyo siku ya Jumapili Aprili 6 mwaka huu na
yeye atawalipa maendeleo na watapata nafasi ya kupanga mipango ya
maendelea kwa ajili ya mafanikio ya Jimbo la Chalinze.
Msanii Dokii akitumbuiza katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Fukayose jana.
Katibu
wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni meneja wa kampeni wa mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia CCM, Bw. Ridhiwani Kikwete
akiwahutubia wananchi katika kata ya Fukayose.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze, Bw. Ridhiwani Kikwete, akizungumza na
kuwapa pole wafiwa wakati alipohani msiba katika moja ya kijiji kwenye
kata ya Fukayose.
Msanii Hafsa Kazinja akitumbuiza katika moja ya mikutano hiyo ya kampeni iliyofanyika kwenye kata ya Fukayose.
Askari
Polisi akiimarisha ulinzi katika mkutano huo huku baadhi ya vijana wa
Kimasai wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali katika mkutano huo.
Mmoja
wa wazee ambaye jina lake halikufahamika mara moja katika kijiji cha
Mtakuja akiwa ameshikilia kipeperushi chenye picha na maelezo ya Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia CCM Bw. Ridhiwani Kikwete.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE)