Mwananchi
juu ya paa la nyumba ya mtu mmoja maarufu kwa jina la Mama Mayunga,
akijaribu kurusha vifuko vya mchanga katika moja ya majengo ya nyumba
iliyozuka moto Jana majira ya saa 5 asubuhi mtaa wa Majengo jirani na
Masangwa Guest House wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Moto
huo unaotajwa chanzo chake kusababishwa na jiko la gesi ulilipuka na
kuiteketeza kabisa nyumba hiyo ikiwa na furniture zake.
Ingawa
jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kuwasihi wananchi kusogea
mbali toka eneo la moto kwani chanzo chake ni moto wa gesi katu watu hao
hawakutii amri hiyo zaidi ya kuusogelea zaidi.
Saa
moja baadaye gari la zimamoto lilifika eneo la ajali ya moto lakini
hata hivyo liliambulia kuzima magofu huku milango, madirisha na mali
zilizokuwa kwenye nyumba hiyo zikiteketea kabisa.
Hali
ndiyo ilivyokuwa huku wananchi hao wa wilaya ya Misungwi wakisubiri
huduma ya zimamoto toka magari ya Halmashauri ya jiji la Mwanza, umbali
wa dakika 45.
(Picha :Wiliam Bundala wa matukiodaima.com kanda ya Ziwa)