Mheshimiwa Ummy Mwalimu alipopata nafasi ya kwenda kumtembelea hospitali shosti yake, Vicky Kamata.
Na Mwandishi Wetu, Dar.
Sakata la Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya UVCCM, Mkoa wa Geita
Vicky Kamata sasa limeingia katika ukurasa mpya baada ya kuzinduka na
kuanza kulilia ndoa yake huku nako wabunge mjini Dodoma wakililia
michango yao.
Kwa
mujibu wa paparazi wetu aliyefika hospitali alipolazwa mbunge huyo ili
aweze kujua hali inavyokwenda na wananchi wanazungumzia suala hilo,
alidadavua kuwa kwa sasa Mbunge huyo amekuwa akililia ndoa yake.
"Yani
kila mmoja anaongea lake kuhusiana na sakata hili ila nimeweza kuongea
na ndugu wa karibu anasema kwa sasa ndugu yao analilia ndoa yake japo
sisi tumesema hatutaki hata kumuona tena huyo mwanaume anayeitwa Charles
maana ndiye chanzo cha yote haya yaliyotokea," alisema ndugu wa karibu
wa Mheshimiwa Vicky huku asitake kutajwa jina lake.
Wananchi
waliongeza kuwa hili lililomtokea mheshimiwa huyo ni dogo tu kufuatana
na mambo ambayo amekuwa akiyafanya, "Sisi Wananchi tunaamini kila
unalolifanya duniani malipo yake ni hapa hapa duniani hakuna haja ya
kuficha ficha mambo... huyu mheshimiwa amezidi kubeba beba waume za watu
na inafikia mpaka anavunja ndoa sasa hili lililomkuta ni fundisho
kwake, ona sasa alivyoumbuka aibu hii ataipeleka wapi??? wananchi hao
walihoji huku wakisema hilo ni fundisho kwa wote wenye tabia kama ya
kwake.
HUKO DODOMA:
Pamoja na
yote yaliyojitokeza, habari zinadai kwamba baadhi ya wabunge
waliochanga pesa ili kufanikisha harusi hiyo tangu juzi wameanza
kuulizia michango yao wataipataje kwa vile harusi basi tena!
“Huku Dom
(Dodoma) hakukaliki bwana. Baadhi ya wabunge wameanza kuulizia michango
yao, wanasema kama harusi haipo basi na chao wakipate,” alisema mbunge
mmoja akiomba kuhifadhiwa jina.
Ndoa ya
Mheshimwa Vicky Kamata na Charles ilikuwa ifungwe Mei 24, 2014 katika
Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza jijini
Dar haikuweza kufungwa kutokana na kuwekewa pingamizi kuwa muoaji
alikuwa ni Mume wa Mama Mwenye watoto 2.