MAKAMU MWENYEKITI WA CCM BARA MZEE PHILIP MANGULA AWASILI MKOANI IRINGA

1
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Iringa Vijijini Mama Delfina Mtavilalu mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa ambapo alipokelewa na baadhi ya viongozi wa mkoa huo na kuelekea moja kwa moja ofisini ambapo alifanya mazungumzo mafupi na viongozi hao na baadae akakutana na waandishi wa habari.
 1a
Akizungumza na waandishi wa habari huku akionyesha moja ya gazeti lililowahi kuripoti kampeni hizo kwa picha Philip Mangula amelaani kampeni alizodai zinadhalilisha watoto zinazofanywa na CHADEMA huku akionyesha mmoja wa watoto ambaye alipigwa picha huku akionyesha sare zake za shule ambazo zimechakaa na kuchanika na mmoja wa wapiga debe wa chama hicho akisema kutangaza umasikini wa mtu ni kumdhalilisha.
 2
Philip Mangula akiingia katika ofisi za mkoa wa Iringa huku akiwa ameongozana na Katibu wa Mkoa wa Iringa Bw. Hassan Mtenga na viongozi wengine.
3
Kipande Cha Gazeti hilo kikionyesha picha iliyochapishwa hivi karibuni inayodaiwa kumdhalilisha mtoto.
4
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akielezea zaidi kuhusu picha hiyo.
  6
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akifafanua zaidi swali la mwandishi huyo.
7
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akielezea mambo mbalimbali yanayohusu uchaguzi huo ambapo amesema CCM ni waumini wa Amani na kwamba katika jimbo la Kalenga hagombei Godfrey Mgimwa bali kinachogombea ni Chama cha Mapinduzi kwani ungekuwa ni ukoo wa mgimwa unagombea basi ungeona akina mgimwa woote wako mbelea wakipiga debe ili washinde lakini kwa sababu ni CCM inagombea ndiyo maana utaona viongozi na wana CCM mbalimbali wakishiriki katika kampeni hizo ili kukipatia ushindi chama chao.
8
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akizungumza nabaadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Iringa kabla ya kuelekea Ifunda ambako atapiga kambi huko.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akizungumza na waandishi wa habari amesema yeye hakkwenda iringa kupiga kampeni kwakuwa kampeni zinapigwa na kamati za siasa pamoja na viongozi mbalimbali kutokana na jinzi walivyopangiwa kazi yake yeye ni kuratibu kampeni hizo na kupokea taarifa za kampeni hizo na kuona kama kamati za siasa za kata zinafanya kazi, Chama cha Mapinduzi kiko katika kampeni jimbo la Kalenga pamoja na vyama vingine kikiwa kimemsimamisha Bw. Godfrey Mgimwa ambapo uchaguzi wa jimbo hilo unatarajiwa kufanyika Machi 16 mwaka huu.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-IRINGA)


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...