MBOTO: SIJAWAHI KUTOKA NA MSANII

MKALI wa komedi Bongo, Haji Salum ‘Mboto’ amesema hajawahi kutoka kimapenzi na msanii mwenzake na hana mpango wa kufanya hivyo.
Mkali wa komedi Bongo, Haji Salum ‘Mboto’.
Akistorisha na Stori Mix, Mboto alisema: “Ni nadhiri niliyojiwekea tangu naanza fani hii. Kamwe siwezi kutoka na msanii mwenzangu. Unajua unapofanya kazi na mtu, anakuwa kama ndugu yako, isitoshe utakapoingiza tu mambo ya mapenzi, hata kazi inaharibika.
“Hao wanaofanya hivyo, wana vipaji vyao bhana, maana mimi naamini kila mtu ana kipaji chake – wengine wana vipaji vya mapenzi. Hata kama mpenzi wangu yupo mbali na anasafiri kila mara, hainifanyi nimsaliti.”


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...