Stori: Mwandishi Wetu
OOHOOO! Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amenangwa kutokana na kitendo chake cha kumwanika laivu mtoto anayeishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).
OOHOOO! Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amenangwa kutokana na kitendo chake cha kumwanika laivu mtoto anayeishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).
Kupitia mitandao ya kijamii, Nisha alitundika picha ya mtoto huyo bila kumziba sura kisha akaandika: “Huyu mtoto ndiyo sababu hasa iliyonifanya nikaja huku, yupo darasa la pili, ana miaka 9, baba yake alimkana akiwa tumboni mwa mama yake, ambaye alifariki pindi tu alipomzaa.
“Jamii inatakiwa ione na kujifunza, inauma sana, ila nipo hapa kwa ajili yake.”
Baada ya hapo, kuna baadhi ya mashabiki wake walimpongeza kwa kuonesha mfano wa kusaidia jamii hasa watoto lakini upo upande wa pili uliomnanga kwa kutojua kuwa kumwanika mtoto wa aina hiyo kunaweza kumwongezea unyanyapaa.
“Ni kweli inauma na Nisha umefanya jambo jema kumsaidia lakini kwa kumwanika hadharani mimi siungi mkono ni bora hata ungemziba. Huku ni kumuongezea unyanyapaa,” aliandika mtoa maoni mmoja.
Mwingine akaandika: “Acha hizo wewe Nisha.
Mbona watu kibao wanasaidia bila kukiuka maadili na haki za binadamu? Kweli kwa upande huo haijatulia.”
Nisha alikwenda visiwani humo katika Kijiji cha Donge, Unguja ambapo alisaidia familia saba ambazo hazina msaada, hata hivyo kitendo cha kumwanika mtoto huyo kilitia doa misaada aliyoitoa ingawa wapo waliosema kuwa inawezekana alifanya makosa bila kufahamu.