Baada
ya mvua kubwa kunyesha jana mkoani Njombe, kituo hiki cha Njombe
kimegeuka matope matupu na kusababisha watumiaji kupata tabu ya kutembea
kwa shida na kutafuta eneo la kukanyaga ili wapite.
Hali halisi kutoka kituo cha mabasi Njombe.
Abiria ambaye jina lake halikujulikana mara moja akipita kwenye matope yaliyosheheni kwenye kituo hicho cha mabasi Njombe.
Ni mwendo wa kuchagua eneo la kukanyaga, wengine wanapandisha suruali zao juu zisipate matope.
Uenda upande huu una afadhali kwa abiria hawa lakini wapi, tope kila mahali.
Tope lenyewe.
LICHA ya tabu hii inayowakumba watumiaji wa kituo cha mabasi Njombe,
ushuru umekuwa ukikusanywa kama kawaida, lakini miezi michache iliyopita
Halmashauri ya Njombe ilitangaza kuwa haina mpango wa kukikarabati
kituo hicho na badala yake imetenga eneo lingine kwa ajili ya kujenga
kituo kipya cha mabasi.
Eddy Blog inaamini kuwa hii adha itaendelea kuwakumba wananchi na
watumiaji wa kituo hiki kwa pamoja hivyo kwa kauli ya halmashauri
inabidi abiria hao wazidi kuwa wapole na kuvumilia hali hii mpaka
kijengwe kituo kipya!