Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimnadi mgombea wa nafasi ya
ubunge jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kwenye
mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Mazizi ambapo alisema
moja ya sifa za mgombea ni kuwafahamu wananchi wake, na wananchi wake
kumfahamu, kufahamu changamoto za wananchi na kufahamu namna ya
kuzitatua changamoto hizo.
Ridhiwani
Kikwete akijinadi kwa wananchi wa kijiji cha Mazizi kata ya Msata
ambapo aliahidi kujenga shule,kusaidia wakina mama na
vijana,kushirikiana na wana Chalinze katika kutafuta ufumbuzi wa
matatizo ya afya,kuinua kilimo,kufanya juhudi za dhati kuboresha kilimo.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Ridhiwani Kikwete akifungua shina la Tonga Road wakati wa ziara za mikutano ya kampeni za ubunge.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha
Tonga wakati wa kumnadi mgombea wa CCM jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani
Kikwete.
Wazee
wa kijiji cha Diozile wakisoma vipeperushi vyenye wasifu wa Ridhiwani
Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge jimbo la Chalinze
zilizofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Lubaya.
Kila
aina ya furaha kwa vijana wa Msoga ambapo mgombea wa Ubunge jimbo la
Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete alifanya mkutano wa hadhara kwa
wananchi wa kijiji hicho.
Karibu
wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wapiga kura wa Ridhiwani Kikwete
wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Msoga ambapo wananchi hao
wamesema kijijini kwao hakutokuwa na kura kwa wapinzani.
Mjumbe
wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Ridhiwani Kikwete akikata utepe
kufungua shina la UVCCM Msoga baada ya kumaliza mkutano wa hadhara wa
kampeni za ubunge.