Home »
Uncategories »
VIJANA WATAKIWA KUWA WABUNIFU NA KUTUMIA FURSA KUJIAJIRI
VIJANA WATAKIWA KUWA WABUNIFU NA KUTUMIA FURSA KUJIAJIRI
Unknown
5:28 PM
Mkurugenzi
Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Sehemu ya Uwezeshaji na Uhamasishaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Kissui Steven
Kissui akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungu rasmi
semina ya Maafisa Maendeleo ya Jamii, Watendaji wa Kata na wakuu wa
vitengo kutoka Manispaa ya kinondoni.Semina hiyo imeandaliwa na Kampuni
ya GODTEC (T) Limited ikiwana lengo la kuwashirikisha wadau katika mfumo
wa Utajirishaji.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Sehemu ya Uwezeshaji na
Uhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.
Kissui Steven Kissui akifafanua jambo wakati akifungua semina ya Maafisa
Maendeleo ya Jamii, Watendaji wa Kata na wakuu wa vitengo kutoka
Manispaa ya kinondoni.Semina hiyo imeandaliwa na Kampuni ya GODTEC (T)
Limited ikiwana lengo la kuwashirikisha wadau katika mfumo wa
Utajirishaji.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya GODTEC(T) Limited Bwana Abnery Shagille
akielezea jambo kwa washiriki wa semina ya wadau wa maendeleo kutoka
Manispaa ya Kinondoni kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi
semina hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sparke International Bwana Gerald
Magooge Reuben akielezea namna alivyofanikiwa kuanzisha kampuni yake kwa
msaada mkubwa wa GODTEC ambapo kupitia mpango wake wa Kiota cha
Utajirishaji uwasaidia vijana kuanzisha miradi ya uzarishaji mali.
Mkurugenzi wa Ubunifu, Uendelezaji na Ufuatiliaji wa GODTEC Bwana
Aloyce Maganga akitoa mada kuhusu namna mfumo wa utajirishaji uanvyo
weza kutekelezwa na wadau wa maendeleo. 
Baadhi ya washiriki wa semina kuhusu namna ya utekelezaji wa mfumo wa
utajirishaji wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inafundishwa na
mmoja wa watoa mada katika (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Sehemu ya Uwezeshaji na Uhamasishaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Kissui Steven
Kissui na viongozi wa GODTEC wakiwa katika picha ya pamoja na Vijana
walioanzisha Kampuni ya Sparke International waliokaa. 
Mkurugenzi
Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Sehemu ya Uwezeshaji na Uhamasishaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Kissui Steven
Kissui akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa semina kuhusu mfumo
wa utajirishaji iliyoandaliwa na Kampuni ya GODTEC (T) Limited.
(Picha / Habari: Frank Shija - WHVUM)
Vijana
wametakiwa kuwa wabunifu na wenye fikra za kimkakati katika kutumia
fursa zilizopo na kujiajiri kwa kutumia taaluma na ujuzi mbalimbali
walionao badala ya kuendelea kusubili ajira za Serikali.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana
kitengo cha Uwezeshaji na Uhamasishaji wa Wizara ya Habari,Vijana,
Utamaduni na Michezo Dkt. Kissui Steven Kissui alipokuwa akifungua
semina ya Maafisa Maendeleo a Jamii na Watendaji wa Kata kuhusu mfumo wa
utajirishaji.
Dkt. Kissui amesema kuwa huu si wakati wa kijana kukaa kijiweni na
kuwataka wabadilike na kuachana na mawazo hasi yanayopelekea kukaa
vijiweni wakisubili ajira za Serikali pekee na kuacha fursa nyingi bila
kutumika.
“Inashangaza sana kumuona mtu ana ujuzi na taaluma nzuru lakini
anakaa kijiweni anasubiri Serikali itangaze kazi, vijana
badilikeni!tumieni fursa zilizopo hapa nchini nanyi mtakuwa mmejikomboa
katika janga la umaskini”. Alisema Dkt. Kissui.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya GODTEC (T) Limited
Bwana Abnery Shagille amesema kuwa vijana wanapaswa kutambua kuwa
Serikali imetimiza wajibu wake wa kutengeneza ajira kwa vijana kwa kuwa
imeweka sera na sheria madhubuti ambazo zinatoa fursa kwa mwananchi
kujiajiri.
Aidha Shagille ameongeza kuwa Kampuni yake imeamua kuchukua jukumu la
kutafsiri sera zilizopo ili jamii ione fursa zilizopo na hatimaye
wachukue hatua ya kutumia fursa hizo badala ya kuendelea kulalamikia
Serikali.
Ameongeza kuwa mpaka sasa kampuni yake imeweza kuwasaidia vijana
waliohitimu vyuo mbalimbali kujiajiri kwa kuanzisha makampuni yao
wenyewe baada ya kupewa mafunzo maalum ambayo utolewa na GODTEC.
Alizitaja kampuni hizo za vijana kuwa ni Sparke International na Brecco
zote za jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo Afisa Mtendaji Mkuu wa Sparke Internation Bwana Gerald
Magooge Reuben ameisema kuwa kupitia GODTEC wamefanikiwa kuanzisha
kampuni hii na kuondokana na tatizo la ajira baadala yake nao wemekuwa
waajiri.
Semina kwa maafisa maendeleo ya jamii, maafisa watendaji wa kata na
wakuu wa vitengo kutoka manispaa ya Kinondoni imeandaliwa na Kampuni ya
GODTEC kwa lengo la kushirikisha watendaji kati mfumo wa uwekezaji
unaojulikana kwa jina la Tajirisha ambao unamuwezesha kijana kumiliki
biashara yake.