ROSE NDAUKA ADAIWA KUMTIBULIA DILI BATULI

Stori:Hamida Hassan na Gladness Mallya
Mastaa wawili, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ na Rose Ndauka wamedaiwa kuwa kwenye bifu chanzo kikidaiwa ni Rose kumtibulia mwenzake dili la ile project ya kusafisha jiji iliyofanyika hivi karibuni.
Malkia wa filamu za kibongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
Akizungumza na Ijumaa kwa sharti la kutotajwa jina lake, chanzo kilisema, wazo la project ile alikuwa nalo Batuli lakini Rose akaingilia kati, hali iliyosababisha Batuli amnunie mwenzake.
Staa wa filamu za kibongo Rose Ndauka
Alipopigiwa Batuli kwanza aling’aka lakini akasema hapendi kuzungumzia mambo hayo kwani yameshapita huku Rose akieleza kuwa, wazo la project hiyo alikuwa nalo kabla hajajifungua hivyo haoni kama kamtibulia Batuli dili lake.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...