SUPER-STAR SHAMSA FORD APATA AJALI

MWANADADA Bongo Movies, Shamsa Ford amenusurika kifo baada ya gari lake kugongana na lingine.
Mwanadada Shamsa Ford.
Akichonga na paparazi wetu, Shamsa alisema tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Sayansi akiwa na gari aina ya Noah aliligonga gari aina ya Vitz na magari yote yakaharibika vibaya lakini bahati nzuri hawakuumia.
“Kweli ni Mungu tu maana ajali ilikuwa mbaya, nashukuru sijaumia ila gari langu ndilo limeharibika vibaya, ilibidi nilifanye ustarabu nikatengeneza magari yote,” alisema Shamsa.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...