Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi,Kamishna msaidizi Renatha Mzinga
Waya zilizokamatwa kwa mtuhumiwa Abdul Mahamud ambazo zimeyeyushwa zinasadikiwa kuwa za kampuni ya simu(TTCL)
..Baadhi ya madawa waliyokamatwa kwa Mtuhumiwa Salum Shaban Mapande
Na Abdulaziz Video, Lindi
Watu
watatu wanashikiliwa na Polisi Mkoani Lindi kwa tuhuma za kukutwa na
madawa ya kulevya aina ya heroin pamoja na Miundo mbinu ya Kampuni ya
simu kinyume na Sheria.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna msaidizi Renatha Mzinga amesema leo
kuwa kwa ushirikiano mkubwa waliopewa na wanajamii wamefanikiwa
kumkamata Bw Salum Shaban Mapande(32)Mkazi wa Dar es sallam akiwa na
madawa ya kulevya kete 42 kubwa na ndogo 104 zenye uzito wa Gram 58 na
pesa taslim tsh 2,827,500 zinazosadikika kuwa za mauzo ya madawa hayo
Watumiwa
wengine waliokamatwa ni pamoja na mwanafunzi wa Chuo cha Utalii mjini
Lindi, Masudi Mohamed(19) aliekutwa na kete 35 za bhangi huku Abdul
Mahamud na Halfan Salum waliokutwa na nyaya za kampuni ya simu TTCL
Zenye Uzito wa kg 5.
Kamanda
Mzinga alisema mkoa wa Lindi umeanza kampeni kubwa ya kupambana na
uhalifu mbalimbali ikiwemo kupambana na wimbi la uingizaji na uuzaji wa
madawa ya kulevya ambalo kwa sasa kuna ongezeko kubwa la utumiaji na
uuzaji wa madawa hayo ikiwemo pombe haramu ya gongo.
Aidha
Kamanda Mzinga ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kujidhatiti na
kufichua wahalifu wakiwemo wauza madawa ya kulevya ambapo Jeshi lake
litatoa ushirikiano na usiri kwa watakaotoa taarifa zinazoashiria
Uvunjifu wa Amani ikiwemo za Usalama barabarani