Anaweza
kuwa ametajwa zaidi kwenye tuzo za KTMA 2014 lakini Diamond Platnumz
hajaliacha Baraza la Sanaa Tanzania likae kwa amani kwa uonevu
ilioufanya kwa Jux, Madee na Snura kutokana na kuziondoa nyimbo zao
kwenye mchakato wa KTMA 2014.
Kupitia Instagram, Diamond ameandika:Ikiwa
kweli tunalengo la kutoipotosha kimaadili jamii yetu na vizazi vyetu
pendwa, nafikiri ni vyema tungeanza kuzuia Video na nyimbo za kutoka
nje, kuliko kuzuia nyimbo na video za nyumbani ambazo uchafu wake
Haufikii hata robo ya uliopo kwenye Nyimbo zinazopewa kipaumbele toka
nje… Hii ni sawa na kuzidi
kuukuza mziki wa nje huku tukiudidimiza na kuua mziki wetu… Will the
target of reaching our goals ever be achieved?? #Ni_Mtazamo_tu.