Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Kigamboni Dk.
Faustine Ndungulile, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Temeke
kwa ajili ya kuanza ziara katika wilaya hiyo leo ikiwa ni siku ya pili
ya ziara yake ya siku nne mkoani Dar es Salaam. Wapili ni Mbunge wa
Temeke Abbas Mtemvu.
Kinana akivishwa skavu baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Temeke
Kinana
akitoka katika ofisi ya CCM wilaya ya Temeke baada ya kuzungumza na
Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo, Wapili ni Mtemvu na kulia ni Mkt CCM
Dsm, Ramadhani Madabida
Kinana
na Madabida wakiwa katika bodaboda ya mwanachama wa VICOBA wakati
Kinana, alipokuwa akienda kwenye mkutano wake na Vicoba Temeke katika
ukumbi wa Kata ya 15 Pub, Temeke
Mtemvu katika bodaboda wakati wa kwenda kwenye kikao hicho na Vicoba wa Temeke
Kinana
akishuka katika bodaboda baada ya kufika kwenye ukumbi wa Kata ya 15
Pub, kwenye mkutano na Vicoba Temeke. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Dar es Salaam. Ramadhani Maadabiba.
Kinana akiingia ukumbini na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke Yahya Sikunjema kwa ajili ya kuzungumza na Vicoba wa Temeke
Vicoba wakimshangilia Kinana alipozungumza nao katika ukumbi wa Kata ya 15 Pub, Temeke
Msanii wa Machozi Theatre Group, akionyesha machejo Kinana alipokutana na Vicoba, Temeke
Mtemvu
akimtuza msanii wa kikundi cha Machozi Theatre Group kikundi hicho
kilipotumbuiza wakati Kinana kizungumza na Vicoba wa Temeke katika
ukumbi wa Kata ya 15 Pub.
Maliki Ndembo (65) akisoma gazeti la Uhuru nje ya ukumbi wa Kata ya 15, Temeka
Kinana
akikagua mitambo ya mradi uliokuwa wa kusafisha gesi kutoka kwenye taka
eneo la Mtoni, Temeke. Mradi wenye mitambo hiyo uliopo chini ya Jiji la
Dar es Salaam, haukuwahi kufanya kazi hadi sasa na sasa Halmashauri ya
wilaya ya Temeke inataka uwe chini ya miliki yake ili iweze kuundeleza.
Kinana
akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick baada ya
kukagua eneo la mradi huo. Picha zote na Bashir Nkoromo