Mtu
mmoja amenusurika kifo kwa kujinusuru katika kichaka katikati ya maji
yanayokwenda kasi akisubiri kuokolewa katika eneo la ruvu mkoani Pwani
baada ya kuzidiwa nguvu na maji alipojitosa kwenye maji kwa nia ya
kutafuta baiskeli yake huku hali ya usafiri ikitarajiwa kurejea katika
hali yake ya kwaiada baada ya maji kupungua huku wakandarasi kutoka
Tanroad wakihangaika kutengeneza maeneo yaliyoharibiwa na mvua.
Wakisumulia
tukio hilo mashuhuda wameiambia TV kuwa mtu huyo alijitosa mwenyewe
kwenye maji kwa nia ya kutafuta baiskeli yake aliyodai imesombwa na maji
na kisha kuzidiwa nguvu na kasi ya maji katika eneo hilo na kisha
kunasa katika kichaka akisubiri kuokolewa huku baadhi ya mashuhuda
wakiwa kando wasijue la kufanya kumnusuru.
Katika
tukio jingine itv imeshuhudia msururu mkubwa wa magari ukisubiri kupita
katika eneo la mto ruvu ambapo baadhi ya wasafiri waliokwama katika
eneo hilo wakielezea tabu wanayoipata pamoja na kuwa na hofu ya kuibuka
maradhi kutokana na wingi wa watu wanaojisaidia hovyo katika vichaka.
Aidha
maji yaliyokuwa yamefunika barabara katika eneo la daraja la mto Ruvu
yamepungua huku magari nayo yakiruhusiwa kupita moja moja wakati
makandarasi kutoka tanroads wakiendelea kukarabati eneo ambalo
lilimong`onyolewa na maji huku eneo zima linalozunguka mto ruvu likiwa
limezungukwa na maji na baadhi ya wakazi wa eneo hilowakioneka kutega
nyavu bila kujali hatari inayoweza kuwapata.
Akizungumza
katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoani Pwani Ulrich Matei
amesema licha ya msongamano mkubwa wa magari hali ya usala katika eneo
hilo ni kubwa kutokana na kupata msaada kutoka kwa vijana wa JKT Ruvu na
kwamba katika kipindi kifupi kijacho hali ya usafiri itarejea katika
hali yake yakawaida.
CREDITS:ITV