Home »
Uncategories »
BIFU ZITO: LULU, JACKLINE WOLPER NA MISS TANZANIA 2012 WAGEUKA PAKA NA PANYA,.. SOMA KISA HAPA UCHEKE
BIFU ZITO: LULU, JACKLINE WOLPER NA MISS TANZANIA 2012 WAGEUKA PAKA NA PANYA,.. SOMA KISA HAPA UCHEKE
Unknown
12:53 PM

E
LIZABETH Michael ‘Lulu’ anayetesa katika filamu za Kibongo, yupo kwenye
bifu zito na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid ambaye
anadai amempora bwana’ke.
Habari zinaeleza bifu lao limefikia hatua ya
kuanikana waziwazi hadi kumwagiana matusi kwenye mitandao ya kijamii,
hasa Instagram lakini huondoa majibizano yao machafu kila baada ya muda
mfupi.
Chanzo
cha habari hizi kinapasha kuwa ugomvi wa Lulu na Husna ni juu ya
mwanaume huyo ambaye anaishi jijini Arusha aliyetajwa kwa jina moja la
Seki anayeelezwa kuwa na pesa za kutosha kusumbua mjini. “Hao
wanamgombea jamaa fulani wa Arusha, anaitwa Seki, ana mawe (pesa) mbaya.
Lakini
wa kwanza kuwa na Seki ni Husna na Lulu alijua, sema Husna na huyo
jamaa walikuwa wanagombana na kumwagana mara kwa mara. Sijui sasa nini
kilimfanya Lulu kwenda kutembea tena na huyo jamaa wakati anajua ni wa
shoga yake, labda ni baada ya kujua wamemwagana,” kilipasha chanzo
hicho.
Baada
ya kupata habari hizi, mwandishi wetu aliwatafuta Lulu na Husna kwa
ajili ya kuthibitisha madai hayo. Lulu alikuwa wa kwanza kupatikana
ambapo alisema: “Jamani mimi simjui kabisa Husna Maulid wala hata katika
fikra zangu hayupo... yaani kifupi simjui.”
Husna alipopatikana
na kuelezwa mkanda mzima, kwanza alishangaa Lulu kutomjua, akasema:
“Hakuna mtu asiyejua kuwa Lulu kanipora mwanaume wangu. Lakini
anajifanya mjanja, tutaoneshana tu. Anajidai sana, anajifanya wa mjini
hanijui mimi, lakini mimi ni wa mjini zaidi yake.”