Staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni wawili hao waliingia kwenye mabishano wakati Steve Nyerere alipokuwa akiandaa .
filamu yake mpya iitwayo Get Out ambapo alipaswa kumshirikisha Batuli.
Ilisemekana kwamba jamaa huyo alipompigia simu, mwanadada huyo alichomoa baada ya kuona makubaliano ya kifedha hayazungumziwi.
Ilisemekana kwamba jamaa huyo alipompigia simu, mwanadada huyo alichomoa baada ya kuona makubaliano ya kifedha hayazungumziwi.
“Batuli
alipohoji kuhusu malipo, Steve hakuweka wazi ndipo mambo
yalipoharibika, kikanuka kisha Batuli akamvaa kwa maneno kiongozi huyo
na kudai hana sifa za kuwa kiongozi,” kilisema chanzo chetu.
Ili
kujiridhisha na madai hayo, mwanahabari wetu alimwendea hewani Batuli
ambapo alipatikana na kukiri kuwa ametofautiana na Steve chanzo kikiwa
ni filamu hiyo.
Mwenyekiti wa Bongo Movies, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’.
“Aliponipigia
simu nilimwambia sitaweza kwenda kushuti kwa sababu hakuna makubaliano
yoyote tuliyofanya ikiwemo gharama, usafiri, mavazi na vinginevyo ndipo
akamaindi na kuanza kulaumu na kisha kukata simu,” alisema Batuli.
Ishu
haikuishia hapo, taarifa zinadai kuwa baada ya Steve kutofurahishwa na
majibu ya Batuli, aliendelea kumtumia meseji za kumlaumu ndipo Batuli
alipochachamaa zaidi kwa kujibu mashambulizi.
“Steve
anapaswa akasomee utawala na uongozi bora kwani hafai kuwa kiongozi,
hana busara, kwa sababu kabla sijagombana naye nilikuwa nikisikia maneno
na majungu ila baada ya ugomvi wangu na yeye nimegundua hafai,” alisema
Batuli na kuongeza:
“Ananiambia
mimi ni msanii mchanga ilihali mimi kwenye kiwanda nipo kwa miaka kumi
na nne na mwaka 2,000 wakati naanza yeye alikuwa anachekesha watu ili
apate kula kwanza nimemdharau kwa sababu amekuwa akinichonganisha na
wasanii wa Bongo Movie eti mimi nimewaambia wanajiuza.”
Baada ya Batuli kufunguka, gazeti hili lilimgeukia Steve Nyerere na kumsomea madai hayo ambapo alifunguka:
“Sipendwi
na watu na sijui nini tatizo, nikiwa kama dairekta nina uwezo wa
kumchagua huyu nifanye naye kazi na huyu kumuacha, yule (Batuli) kama
analeta chuki basi zitakuja hivyo basi ni nyingi tu,’’ alisema Nyerere
na kuongeza:
“Kwa
heshima niliyoitengeneza kwa miaka 32 alafu nije nigombane na mwanamke,
kwanza nagombana naye nini? Nashukuru nimepata ushauri, naendelea na
kazi ya kutetea maslahi ya Bongo Muvi kama ni filamu mimi
nilishachezesha msanii mwengine.”
>>GPL