NI NGUMU KUAMINI LAKINI BAADA YA MIAKA 10 HATIMAYE KUNDI LA P-SQUARE KUTOKA NCHINI NIGERIA LAFARAKANA.....!!!

Nilikuwa naskia sikia tu Stori zinazowahusu Peter and Paul Okoye wa kundi la P Squre wakiwa na matatizo kwa sasa. Ni kwamba wamekuwa hawaelewani hivi sasa katika kila kitu... Nyimbo, Videos na Hata Kimawazo pia Lakini kwa sababu ya Kuwa Mapacha nilidhani wataweza kumaliza Tofauti zao na kukaa pamoja kama zamani... Hivyo Sikuweza Kuandika chochote.

Siku ya Alhamis 16/04/2014 niliweza kupata habari nyingine kutoka kwa chanzo makini kuwa Ma kaka Hao wamezichapa kavukavu katika kipindi cha Mazoezi yao. Wanataka Kutengana na Madancers wao Huu ni Ukweli lakini niliamua kuiacha stori hiyo kama ilivyo kwa sababu hawa ni Ndugu na Ndugu wanapokosana Baadae hupatana, Lakini Kwa sasa Kaka Yao Mkubwa Jude Okoye ambaye ndiye Manager wao aliweza Kuandika Katika Ukurasa wake wa Twitter hivi: "After ten years he's done" Hii inamaanisha ukweli wa mambo haya na yameshindikana kurekebishika na kuamua Kujigawa kila Mtu awe kivyake.
Chanzo kinasemekana ni Mke wa Mmoja kati yao ndio aliyefanya Makaka Hawa Kugombana. 
Kwenu P Squre Ninaomba Msifikirie Hata siku Moja Kutengana kwani Mtaweza Kuumiza Mioyo ya watu Wengi sana Hapa Duniani...Nikiwa na Mimi ni Mmoja wao Tafadhali Kuweni Pamoja.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...