BILA
mchezaji bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo, Real Madrid wanaingia kata
EL CLASICO ya 3 na ya mwisho kwa Msimu huu dhidi ya FC Barcelona usiku
wa leo katika uwanja wa Estadio Mestalla Mjini Valencia.
Hii ni fainali ya Fainali ya Kombe la Mfalme, Campeonato de España – Copa de Su Majestad el Rey, kwa kwetu limezoeleka kwa jina la Copa del Rey.
Barcelona,
ambao wameshatwaa Kombe hili mara 26, mara ya mwisho kulitwaa ni 2012,
wakati Real, ambao wamelitwaa mara 18, Mwaka Jana walifungwa katika
mechi ya fainali na mahasimu wao Atletico Madrid.
Barca
na Real zimeshakutana mara mbili Msimu huu kwenye mechi za ligi kuu
maarufu kama La Liga, huku Barca wakishinda Mechi zote mbili.
Mara
ya mwisho kukutana kwenye Copa del Rey ni Mwaka 2011, tena Uwanja huu
huu wa safari hii, Estadio Mestalla, ambapo Bao la Dakika za Majeruhi la
Cristiano Ronaldo liliwapa Kombe Real na pia kumpa Kombe la Kwanza
Kocha Jose Mourinho kwenye himaya yake na Real Madrid.
MECHI 3 ZILIZOPITA:
-Real 3 (Benzema 2, Ronaldo) Barcelona 4 (Iniesta, Messi 3), La Liga, Machi 2014
-Barcelona 2 (Neymar, Sanchez) Real 1 (Jese), La Liga, Oktoba 2013
-Real 2 (Benzema, Ramos) Barcelona 1 (Messi), La Liga, Machi 2013
Lakini
safari hii kila Klabu ina Meneja mpya, Carlo Ancelotti na Real na
Gerardo Martino kwa Barca, na wanatinga kwenye Fainali hii wakitokea
kwenye matokeo tofauti kabisa.
Barca
wanatinga Fainali hii wakiwa kwenye majonzi makubwa kwani Wiki moja
iliyopita walikuwa kwenye ndoto kubwa ya kutwaa Trebo kama walivyofanya
Mwaka 2009 lakini mambo yakapinduka na wakatolewa toka UEFA na Atletico
Madrid na Siku 3 baadae kufungwa 1-0 na Granada kwenye La Liga na
kuachwa wakiwa Pointi 3 nyuma ya Vinara Atletico na Real huku Mechi
zikiwa zimebaki 5.
Tofauti
kabisa, Real wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa na morali ya juu baada
ya kufuzu kuingia Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na pia kuwa
kileleni mwa La Liga, pamoja na Atletico, baada ya kuifumua Almeria 4-0
Siku 3 baadae.
Kila
Timu inakabiliwa na Majeruhi wengi huku Barca ikiwa dhoofu kwenye safu
yao ya ulinzi wakiwemo Gerard Pique, Carles Puyol na Marc Bartra, ambaye
kidogo ni nafuu na huenda akacheza, lakini upo uwezekano mkubwa kwenye
Mechi hii Difensi ya Barca ikawa na Viungo, Mascherano na Busquet, kama
Masentahafu wao.
Real
wataingia wakiwa na hatihati kuhusu kucheza kwa Staa wao Cristiano
Ronaldo ambae hajacheza Mechi 2 zilizopita akiwa na maumivu.
Carlo
Ancelotti ameleeleza jana kuwa Ronaldo hatakuwepo, lakini kukosekana
kwake kunaweza kutoa mwanya kwa ama Asier Illarramendi au Isco kucheza
na kuungana na Angel di Maria, Gareth Bale na Karim Benzema kwenye
mashambulizi.
Ancelotti
mapema jana alikaririwa akisema Ronaldo anaweza kucheza kwasababu
anaendelea vizuri, lakini baadaye kwenye mkutano na waandishi wa habari
kabla ya mechi ya leo alithibitisha kuwa nyota huyo atakosekana kabisa.
“Cristiano Rinaldo hatakuwepo, lakini tuna wachezaji wengi katika kikosi chetu”.
“Tuna
imani kubwa na timu hii. Nimekuwa nikijitahidi kukabiliana na majeruhi
na nadhani tutafanya kazi nzuri tu”. Aliongeza kocha huyo raia wa Italia
ambaye hata hivyo aligoma kutaja kikosi kinachoweza kuanza leo hii.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Real Madrid: Casillas; Carvajal, Ramos, Pepe, Coentrao; Modric, Alonso, Illarra; Di Maria, Benzema, Bale
Barcelona: Pinto; Alves, Mascherano, Bartra, Alba; Busquets, Xavi, Iniesta; Neymar, Messi, Sanchez
COPA del REY-NJIA YA FAINALI
NUSU FAINALI
Marudiano
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi 2]
Jumanne Februari 11
Atletico de Madrid 0 Real Madrid CF 2 [0-5]
Jumatano Februari 12
Real Sociedad 1 FC Barcelona 1 [1-3]
FAINALI
Aprili 16
Real Madrid v Barcelona