GAMBIA YAJITANGAZA KUWA TAIFA LA KIISLAMU AFRIKA, RAIS PROFESSA YAHYA A.J.J AWAPA SALAMU MABONYENYE WA MAGHARIBI

BANJUL, Gambia

RAIS wa Gambia, Sheikh Professor Alhaji Dr. Yahya A.J.J. Jammeh, GMRG, FAAICL ametangaza nchi yake kuwa miongoni mwa nchi za Kiislamu na lugha ya kwanza ya nchi hiyo kuwa Kiarabu.


Rais Jammeh akibadilishana mawazo na wananchi wake.
 
Nchi ya Gambia ipo upande wa Magharibi mwa Bara la Afrika ambapo rais huyo amesisitiza kuwa lugha ya kwanza ya nchi hiyo itakuwa kiharabu.

Mwandishi wa mtandao huu aliyepo mjini Banjul anasema kuwa, Rais huyo ametoa amri kwa wananchi wa nchi hiyo kuwa shule zote na vyuo vya nchi ya Gambia vinapaswa kufundisha masomo kwa lugha ya kwanza ambayo ni Kiarabu,huku akipitisha muswada kwenye Bunge la nchi hiyo kuwa katika nchi ya Gambia Lugha ya kwanza itakuwa Kiarabu.

Baraza la Mawaziri wa nchi ya Gambia lilifanya kikao cha dharura siku ya Ijumaa iliyopita katika mji mkuu wa nchi hiyo Banjul wamepitisha kwa kauli mmoja kuwa lugha ya kwanza ya nchi hiyo itakuwa ni Kiarabu na lugha ya pili ni Kiingereza.

Hata hivyo, utawala wa Gambia umetangaza kujitoa kuwa mwanachama wa nchi zilizofanywa au zilizokuwa koloni la Mwingereza.

"Gambia inatangaza kuwa lugha ya kwanza itakuwa ni Kiarabu,na pia imejitoa rasmi kuwa mwanachama wa nchi zilizofanyiwa ukoloni na Mwingereza na hatua hiyo ni mwanzo wa kuelekea kuwa Serikali au dola la Kiislamu," ilisema sehemu ya taarifa iliyochapishwa na jarida la The Press Afrika.

Rais huyo katika miaka ya hivi karibuni alikuwa na mahusiano mazuri na baadhi ya mataifa ya Kislamu kama vile nchi za kiarabu huko akiwa ametekeleza ibada yake ya Hijjah kwa mara mbili.

Duru za kuaminika zinaeleza kuwa Ikulu ya nchi hiyo itabadishwa jina na kuitwa kuwa "Ufalme wa Jamhuri ya Kislamu ya Gambia" uamuzi wa Rais wa Gambia unadaiwa umeyakasirisha sana mataifa ya nchi za Magharibi.

Bunge la Muungano wa nchi za Ulaya umetangaza vikwazo dhidi ya Gambia na kuamuru kuwekewa vikwazo vya fedha zilizopo kwenye benki za Ulaya.

Gambia ni miongoni mwa nchi ndogo zilizopo Magharibi mwa Bara la Afrika na inapakana na nchi ya Senegal na uchumi wa nchi hiyo mara kadhaa ulionekana kuwa chini.


Hata hivyo, Kanisa Katoliki la nchini Gambia nalo limekasirishwa na hatua ya Rais wa Gambia na itakumbukwa asilimia kubwa ya watu wa Gambia ni Waislamu, lakini kwa muda wa miaka mingi Mataifa ya Magharibi yalikuwa yakikataa Gambia kuwa miongoni mwa nchi za Kiislamu.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...