Umati wa watu waliofika katika eneo la kitanzini kuangalia handaki hilo
Handaki la ajabu limeonekana katika eneo la kata ya kitanzini mtaa wa sokoni Katika tukio hilo lililokuwa gumzo kubwa katika eneo hilo huku kila mmoja akisema lake Mtandao huu ulipokutana na mmiliki wa nyumba hiyo hakuweza kuwa na majibu yakuridhisha huku akisema yeye hafahamu shimo hilo limetokea wapi.
Handaki hilo
ambalo lilionekana jana na wachimbaji wa mitaro wa JR wanaoshuhulika na
uwekwaji wa mabomba mapya ya maji safi wanaeleza katika kuchimba ndipo
walipokutana na chemba hiyo ikiwa imefunikwa na kudhani kuwa inatumika
kama shimo la choo ya nje lakini haikuwa hivyo maana lilikuwa wazi
limejengewa na hakuna dalili ya kutumika kama choo.
Mkuu wa Wilaya Ya Iringa mjioni Dkt Leticia Warioba akihojiana na mmiliki wa nyumba ambayo handaki hilo limeonekana
Mkuu wa Wilaya afika eneo la tukio:
Mkuu wa wilaya ya Iringa Dkt Leticia Warioba akafika katika eneo la tukio huku akiwa na wa wafanyakazi wa Kampuni ya JR pamoja na afisa wa usalama ambao waliishia kuangalia njia hiyo pasipo kuingia ndani ya handaki hilo.
Nini maoni ya wakazi waliofika katika eneo hilo?
Wengi wa wakazi waliofika katika eneo hilo hawakusita kueleza hisia zao huku wengine wakieleza labda ni mahandaki yaliyokuwa yakitumiwa na Wajerumani enzi za ukoloni, huku wengine wakieleza labda handaki hilo limekuwa likitumiwa na majambazi kama sehemu za kujificha na kuhifadhia mali walizoiba japo hapakuonekana na mali aina yeyote.
PICHA NA FRANCIS GODWIN