VIDEO
queen’ wa Kibongo, Agness Gerald, ‘Masogange’, amefunguka kuwa
aliyempa mzigo wa unga na akakamatwa nao nchini Afrika Kusini, alikuwa
amevalia kininja, hali iliyomfanya ashindwe kumtambua.
Taarifa
za uhakika kutoka vyanzo vyetu makini katika kikosi kazi cha kuzuia na
kudhibiti madawa ya kulevya nchini (Task Force), zinasema kuwa
mwanadada huyo alipofika katika nchi hiyo, alipigiwa simu na mtu ambaye
hamjui aliyemwambia kuwa atapewa mzigo, hivyo ajiandae kuupokea.
‘Video queen’ wa Kibongo, Agness Gerald, ‘Masogange’.
“Alidai
kuwa kuna mtu aliyevalia kininja alifika eneo alilokuwepo uwanjani pale
ambaye hakumsemesha badala yake alimpatia mzigo wa unga ambao ulikuwa
kilo 150 ambao hapa kwetu ni madawa ya kulevya na kuondoka
kusikojulika,” kilisema chanzo.
Kwa
upande wake, Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya
nchini, Godfrey Nzowa alipohojiwa na gazeti hili alithibitisha kuwa
Masogange aliwaeleza polisi wa Afrika Kusini kuwa aliyempa unga ule ni
mtu aliyekuwa amevalia kininja.
“Unajua watu hawa wanaojihusisha na madawa ya kulevya wana mbinu nyingi na wamekuwa wamejiandaa kwa lolote litakalotokea. Naamini alisema vile ili kukwepa kushurutishwa kumtaja aliyempa.
“Aliwaambia
kuwa mtu huyo alimpa mabegi yale palepale uwanjani na hawezi kumtambua
kwa sura labda kwa fulana aliyokuwa amevaa kwa sababu alikuwa amevaa
kininja,” alifafanua Kamanda Nzowa.
Alisema
unga huo ulifanyiwa uchunguzi kwa mkemia mkuu wa serikali wa nchi hiyo
na ikagundulika kuwa si Crystal Methamphetamine bali ni Ephedrine ambayo
si unga ila ni kemikali hatari ambayo ikichanganywa na dawa nyingine
hupatikana unga halisi wa madawa ya kulevya.
Aliongeza
kuwa, mtu yeyote akikamatwa na malighafi kama hizo hapa nchini
adhabu yake haizidi faini ya shilingi milioni 5 au kifungo cha miaka 30
ama zaidi.