Mkuu
wa wilaya ya Ulanga Mh. Fransis Miti amesitisha huduma ya kivuko kati
ya ulanga na kilombero kwa kutumia pantoni ya kivuko MV. KILOMBERO hadi
hapo maji yatakapo pungua kutokana na kivuko hicho kuzidiwa na nguvu ya
maji.
Amewaomba
wananchi wa wilaya zote mbili kuto kusafiri kwa muda kwa safari zisizo
za lazima hadi hapo maji yatakapo pungua huku kwa wale wanao lazimika
kusafiri sasa kutumia boti ndogo zilizopo na kuacha kutumia mitumbwi
ambayo si salama.
|
hatariii |
Wakati
huo huo maji hapo juzi jioni yalikata mawasiliano ya barabara kati ya
Ulanga na kilombero kwa kuzoa moja ya kalavati upande wa Ifakara ambapo
moja ya gari lilisombwa na maji huku nayo pantoni ilisitisha huduma
kwamuda baada ya kusombwa na maji na kupelekwa upande wa bondeni.
Mitumbwi
na boti ndogo zilionekana zikivusha watu hapojuzi huku nauli katika
boti na mtumbwi wa kawaida kwa mtu mmoja ikipanda kutoka shilingi 200 ya
kawaida hadi 1000 kwa mtu mmoja huku pikipiki zikisafirishwa kwa kati
ya shilingi 3000 hadi 8000.
baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi hapo juzi katika eneo hilo
la kivukoni wamesema hali mbaya ya usafiri inayojitokeza sasa
nikutokana na uzembe wa kutoyatengeneza makalavati hayo katika msimu wa
kiangazi huku mamlaka inayohusika na utengenezaji wa barabara katika
eneo hilo ikiendelea kukwangua tuta la barabara hiyo lililo wekwa na
campuni ya BENACO miaka hiyo, hali iliyopelekea tutahilo kuwa dhaifu.
Wakati hayo yakiendelea leo imeripotiwa moja ya mchina amejinyonga,
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana zinadai mchina huyo aliyekuwa
anahusika na michoro ya ujengaji wa daraja amejinyonga kutokana na
upweke uliokuwa unamsibu.
baadhi ya watu wakaribu na vibarua wa ujenzi wa daraja la mto kilombero
ambalo bado halija anza kujengwa hadi sasa licha ya kutakiwa kukamilika
mwakani wamesema yawezekana mchina huyo amejinyonga kutokana na hali
mbaya iliyojitokeza kutokana na kuzama kwa makaravati ambayowalikuwa
wamekwisha jenga.
mvua za mwaka huu katika
wilaya ya kilombero na Ulanga zinadaiwa kuwa ni kubwa kuwahi kutokea
ambapo miundombinu ya barabara iomehalibiwa vibaya.
|
Barabara kutoka lupiro kwenda mahenge eneo la Fimbo |
|
Mto Kilombero |
|
Muendesha Mtumbwi Kazini |
|
Moja ya usafiri unaotumika |
|
Moja ya karavati yaliyojengwa na wachina |
|
Karavati jipya |
|
Eneo la barabara Kivukoni upande wa Ifakara |
|
Kalavati likiwa limezamishwa na maji |
|
Kalavati likiwa limemeguka upande |
|
Foleni ya Magari Kabla ya kufikiakivukoni |
|
Katapila likiwa limewekwa katikati ya barabara kuzuia njia watu wasipite kutoa nafasi ujenzi uendelee. |
|
kivukoni- hali halisi |
|
eneo liliosombwa na maji na kuvunja mawasiliano yaUlanga na Kilombero |