Mwanafunzi
wa Eden Hilling College aliyetajwa kwa jina la Atu Gabriel amefariki
akidaiwa kujaribu kutoa mimba kwa kunywa vidonge.Kwa mujibu wa Kamanda
wa Polisi mkoa wa Pwani (RPC), Orech Mtei, katika kuthibitisha kutokea
kwa tukio hilo, alisema Jumamosi April 26 mwili wa Atu ulikutwa katika
chumba cha mwanaume aliyefahamika kwa jina la Hafidhi ambaye anadaiwa
kuwa mpenzi wake.Kamanda Mtei ameeleza kuwa polisi walikuta mwili wa
marehemu ukiwa karibu na vidonge alivyotumia huku akitokwa damu nyingi
sehemu za siri na kwamba polisi wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa Hafidhi
ambaye alidaiwa kukimbia baada ya tukio."Ni kweli tukio hilo limetokea
Jumamosi Aprili 26 mwaka huu eneo la Kwa Mfipa baada ya jeshi letu
kutaarifiwa kuwepo kwa mwili huo na polisi walipofika na kufanya
uchunguzi wake tulibaini marehemu alifariki dunia kaika jaribia la
utoaji wa mimba.....hata hivyo mwili bado upo Hospitalini Tumbi kwa
ajili ya uchunguzi zaidi," alisema Kamanda Mtei.
Kamanda
Mtei alisema mara baada ya kutokea kwa tukio hilo, kijana aliyetajwa
kwa jina la hafidhi ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake alitokewa eneo
la tukio na jeshi hilo kwa sasa linamtafuta kwa ajili ya mahojiano zaidi
kabla ya kufikishwa mahakamani.
"Baada
ya tukio mtuhumiwa alikimbia na hadi sasa bado haijulikana alipo, jeshi
letu linaendelea kumtafuta popote alipo na mara baada ya kumpata
tutamuhoji na baadae atafikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua za
kisheri," alisema Mtei.
Secretary
wa Eden Hilling College ambaye hakutaka jina lake litajwe alieleza kuwa
mwanafunzi huyo aliaga chuoni hapo siku ya Alhamisi kuwa anakwenda
katika hospitali ya Mwananyamala kumuuguza wifi yake na kwamba
wamesikitishwa sana na habari ya kifo cha mwanafunzi huyo.
"Aliaga
vizuri tu siku ya Alhamisi kwamba anauguliwa na anakwenda kumuuguza
wifi yake aliyelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala lakini Jumamosi
ndio tukapokea taarifa za kifo chake! Hii inaonyesha huyu mwanafunzi
aliudanganya uongozi wa Chuo kitu ambacho hakikuwa sawa kabisa,"
Alisema.
Alisema hivi sasa uongozi wa Chuo unawasiliana na wazazi wake waliopo Makambaku kwa ajili ya kuja kuuchukuwa mwili wa marehemu.
Kwa
undani wa habari hii na kusikiliza alichokisema RPC wa Pwani, ndugu na
jamaa wa marehemu na majirani katika nyumba aliyokutwa wakisimulia tukio
hilo, usikose kusikiliza Hatua Tatu ya 100.5 Times Fm Leo (April 28)
katika kipengele cha Habari Ndio Hiyo na Maryam Kitosi, Edson Mkisi Jr
na Dj R Guy.
Kipindi
cha Hatua Tatu kinakuwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa tatu
kamili asubuhi hadi saa sita kamili na Maryam Kitosi, Edson Mkisi Jr. na
Dj R Guy.