Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 16 amenusurika kifo kwa maajabu baada ya kujificha na kusafiri katika gurudumu la ndege iliyokuwa ikielekea mjini Carlifornia kutoka Hawaii nchini Marekani.
Karibu robo ya watu wote wanaosafiri wakiwa wamejificha katika gurudumu la ndege hufariki |
Safari hiyo ilidumu kwa saa 5.
Hali
yake inadaiwa kuwa shwari licha ya vipimo vya juu vya baridi baada ya
ndege hiyo kusafiri juu ya bahari ya Pacifiki kwa saa tano.
Msemaji
wa shirika la ndege la Hawaii, alisema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo
walimuona kijana huyo baada ya ndege kutua Jumapili asubuhi.
Alihojiwa na FBI na kupewa huduma ya dharura huku wauguzi wakisema afya yake iko shwari.
Mvulana huyo anasemekana kutoroka nyumbani na kuruka ukuta katika uwanja wa San Jose ili kuweza kusafiri kwa ndege hiyo.
alisema masemaji wa shirika hilo la ndege.
aliongeza kusema msemaji wa shirika la FBI.
Inaarifiwa punde tu baada ya ndege kutua, kijana huyo alishuka na kuanza kurandaranda katika uwanja wa ndege.
Kijana huyo alipatikana tu akiwa na kichana mkononi.
Aliponea sana, maana alikosa hewa huku akipigwa na baridi kali ndege ilipokuwa inaruka mita 12,000 juu angani.
Kadhalika kijana huyo anaarifiwa kupoteza fahamu muda wote wa safari.