Gari
aina ya Nissan Hard Body ambayo namba zake yake ya usajili haikuweza
kufahamika mara moja ikiwa imeharibika vibaya mara baada ya kusababisha
ajali ya kugongana uso kwa uso na daladala katika eneo la Suye, Barabara
ya kuelekea Moshono mjini Arusha
Daladala
iliyogongana na Gari aina ya Nissani Hard Body muda mufi uliopita
katika eneo la Suye barabara inayoelekea Moshono Mjini Arusha
Daladala zilizogongana zikiwa zimetoka kabisa nje ya barabara mara baada ya ajali hiyo kutokea katika eneo la suye.
Polisi
wakiwa wamefika Eneo la tukio kwaajili ya kuhakikisha usalama na amani
inakuwepo mara baada ya ajali hiyo kutokea.Picha zote na mdau Emmanuel
Lukwaro
Ajali
mbaya imetokea MjiniArusha katika eneo la Suye, barabara ya kuelekea
Moshono, Ajali hiyo imehusisha magari aina ya Hice na Nissani Hard Body,
na kupelekea Dereva wa daladala kuvunjika vibaya miguu yote miwili
kutoka na magari hayo kugongana uso kwa uso.
Ajali
hiyo imesababishwa na Dereva wa Nissani Hard Body ambaye alikuwa amelewa
na kupelekea kuyumbayumba barabarani na hatimaye kuigonga daladala.
Katika
Hali isiyo ya kawaida dereva wa Nissani Hard Body ambaye amesababisha
ajali hiyo alipokua akijaribu kukimbia alitoa bastola kwaajili ya
kuwatishia watu wasimzuie na ndipo kizaa kilipotokea na kusababisha
barabara hiyo kufungwa kwa muda na kusababisha umati mkubwa wa watu
kushuka kwenye magari na kulizunguka eneo hili.
Hata hivyo polisi waliweza kufika eneo hilo la tukio na kuweza
kumdhibiti dereva wa gari aina ya Nissani Hard Body ambae amesababisha
ajali hiyo na hatimaye hali ya utulivu imerejea.