WATU WATATU MBARONI KWA KUKUTWA NA BANGI NDANI YA BASI MKOANI DODOMA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia abiria wa tatu waliokuwa wakisafiri na Basi la New Force kutoka Kahama kuelekea Jijini Dar es Salaam.
Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime, wamekamatwa leo mchana wakiwa wanasafirisha Debe ishirini za bangi.Wanaoshikiliwa ni Kevin Prospar(aliyekaa pichani kulia),Joseph Charles (aliyekaa kulia) na John Joseph(aliye kaa katikati)
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime kushoto akikagua bangi iliyo kamatwa.
Basi la New Force lililokamatwa likiwa limebeba abiria waliokuwa na bangi likiwalimeshililiwa kwa muda Makao ya Polisi Mkoa wa Dodoma.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...