ANGALIA PICHA KIJANA NUSURA KUFA BAADA YA KUIBA NGURUWE UKO MOSHI

 

KATIKA kuelekea sikuu za Krismasi na Mwaka mpya pilika pilika zimeongezeka katika mji wa Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla huku vibaka pia wakiendelea na udokozi na wizi wa vitu mbalimbali.
Katika kuthibitisha hilo juzi Tanzania Daima limeshuhudia mkazi wa kijiji cha Nshara, Machame wilayani Hai,ambaye jina lake halikupatikana mara moja amenusurika kuuawa kufuatia kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kumshambulia kwa silaha za jadi baada ya kuiba kitoto cha nguruwe maarufu kama "Kiti moto".
Tukio hilo la aina yake ambalo linaashiria maandalizi ya siku kuu hizo lilitokea juzi majira saa 5.30 asubuhi kijijini humo baada ya mkazi huyo kuonekana akiwa amembeba mnyamya huyo begani akiwa katika mfuko,maarufu kama Sandarusi mithili ya mzigo wa kawaida.
Akizungumzia tukio hilo,mkazi wa kijiji cha Nshara, Husein Mbaruku alisema mtu huyo alionekana akinyata katika banda la Nguruwe akiwa na mfuko wake akiamini kuwa hakuna mtu aliyemuona ingawa wenyeji nao walikuwa wakimvizia ili kuona anachotaka kufanya.
"Huyu bwana ni mwizi mzoefu katika eneo hili ,mara kwa mara wenyeji hapa wamekuwa wakilalamika kuibiwa nguruwe wao leo naona Arobaini yake imefika ,wananchi wamemkamata na ndio hivyo kama unavyoona kapigwa sana"alisema Mbaruku.
Alisema mtu huyo alifanikiwa kuiingia katika banda la nguruwe na kukikamata mmoja ya kitoto cha nguruwe ambacho wakati wa harakati ya kuingizwa katika mfuko huo kilipiga kelele ambazo ziliwashitua majirani wengine.
Kutokana na mazingira hayo,mtuhumiwa huyo alikuwa mjasiri na kukimbia nacho hivyo hivyo jambo lililosababisha baadhi ya wananchi kuanza kumfukuza kwa kasi ndipo alipoanguka eneo la mfoni ambapo wananchi walimjeruhi kwa silaha hizo ikiwamo mawe.
Katika hali isiyo ya kawaida huku mtuhumiwa huyo akivuja damu nyingine mmoja wa raia alitaka kumchoma kwa gurudumu la gari ndipo wananchi wenzake walipoingilia kati na kumuokoa mtuhumuwa huyo ambaye alipelekwa kituo cha polisi bomangombe.
Hadi kipindi hiki kinaondoka eneo la tukio majira ya saa saba mchana mtuhumiwa huyo alikuwa hajitambui kutokana na kipigo hicho kutoka kwa raia ambao baadaye walitawanyika baada ya kuhisi wamefanya mauaji. 
Mkazi wa kijiji cha Nshara Machame akivuja damu baada ya kupokea kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali kufuatia wizi wa mtoto wa Nguruwe,tukio hilo lilitokea juzi wilayani Hai.Picha na Dixon Busagaga


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...