MSANII wa filamu Bongo, Elizaberth Michael ‘Lulu’ hivi karibuni aliwashangaza watu baada ya kuvukwa na gauni alilokuwa amevaa na kulazimika kutembea huku sehemu kubwa ya kifua chake ikiwa wazi.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika kiwanja
kimoja kichopo mjini Arusha ambapo mmoja wa watu aliyemtia machoni Lulu
aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema:
Msanii wa filamu Bongo, Elizaberth Michael ‘Lulu’.
“Yaani nilimuona Arusha akiwa amevaa gauni lililoacha wazi matiti yake,
kaficha chuchu tu na inavyoonekana gauni lilimvuka, akaonekana akihangaika kulirudishia bila mafanikio.”
Ijumaa
lilimtafuta Lulu kupitia simu yake ya mkononi bila mafanikio ila
juzikati akatundika picha kwenye mtandao wa instagram akiwa amevaa gauni
kama lile aliloonekana nalo Arusha.