Eduardo Vargas akishangilia bao la kuongoza la Chile dhidi ya Hispania kombe la dunia.
Vargas akianguka chini baada ya kupiga mpira na kumuacha Iker Casillas akiambulia manyoya tu.
MABINGWA
watetezi wa kombe la dunia wafungasha virago rasmi!. Hispania
wameondoka. Wao na Australia wamekuwa wa kwanza kuaga mashindano hayo
kimahesabu, kiroho na kimwili.
Ushindi uliostahili kwa Chile kwenye
dimba la Maracana umeiacha timu ya Vicente Del Bosque ikiwa haina ujanja
wowote. Hakika kiwango cha Chile katika mechi hii kinaonesha maendeleo
ya mpira.
Swali ni kwamba ufalme wa Hispania umefika kikomo kwa matokeo haya?.
Chile
wameshinda, sio kirahisi, lakini vizuri. Mabao mawili ya kipindi cha
kwanza, yamewasumbua Hispania kipindi kizima cha pili, lakini hawakuweza
kusawazisha.
Diego Costa alikosa nafasi nzuri na nafasi kama hiyo aliipoteza Sergio Busquet.
Dakika
za mwisho, Mauricio Isla angefunga bao la tatu kwa chile. Timu hiyo ya
Amerika ya kusini ilicheza mpira vizuri na kuendana na kasi ya Hispania.
Kazi
waliyofanya Chile ilikuwa nzuri, jinsi walivyotumia nafasi na namna
walivyokaba, ilikuwa silaha tosha ya kuwashinda Hispania.
Kipigo cha mabao 5-1 walichopata kutoka kwa Uholanzi kiliwapunguzia imani Hispania, ilikuwa ngumu kupata matokeo.
Ulikuwa mchezo ambao Hispania wanahitaji ushindi ili kuendelea kuwepo katika michuano hii.
Kipa
wa Chile, Claudio Bravo aliokoa mchomo wa Iniesta zikiwa zimesalia
dakika 6 mpira kumalizika na hapo jahazi la Hispania lilizama dhahiri
shahiri.
Safu mbovu ya ulinzi katika mechi mbili, imeiua Hispania na kuvuma matokoe ya hovyo.
Gozi kambani: Kipa wa Real Madrid hakuwa na la kufanya.
Oyooooo!: Lakini Casillas angeweza kumdhibiti Charles Aranguiz
Casillas aliweza kuokoa mpira wa adhabu tu uliopigwa na Alexis Sanchez.
Aranguiz aliupiga mpira kwa ufundi mkubwa na kuuzamisha nyavuni
Goooo! wachezaji wa Hispania walijikusanya baada ya kupigwa bao la pili
Majanga babu weee, chezea Chile! Vicente Del Bosque kibarua chake sasa kipo hewani.
Upewe nini Sergio Busquets , hii ilikuwa nafasi yako kufunga kaka!
Vitu vya hatari!: Hii ilikuwa pasi ya maajabu ya mshambuliaji ambaye muda si mrefu atakuwa Chelsea Diego Costa