Vurugu
kubwa zimetokea katika kijiji cha Buyango wilayani Muleba mkoani Kagera
baada ya wazazi kuikataa maiti ya mtoto wao kwa madai amenyofolewa
viungo vyake vya mwili hali iliyosababisha polisi kutumia mabomu ya
machozi kutawanya makundi yaliyofunga barabara na kubomoa chumba cha
kuhifadhia maiti kutafuta viungo hivyo.
Vurugu
hizo zimetokea baada ya mama mmoja mkazi wa Arusha aliyepeleka maiti ya
mtumishi wake wa ndani na kuwakabidhi wazazi wake kwa masharti ya
kutoifunua hali iliyosababisha mtafaruku mkubwa ambapo mama huyo
amelazimika kwenda hospitali kukabidhi mwili huo ambapo baadhi ya ndugu
na jamaa walivamia chumba cha kuhifadhi maiti na kubomoa mlango kisha
waka angalia mwili ambao wameukuta ukiwa na majeraha na kwamba haufanani
na binti yao aliyefahamika kwa jina la Ajela Tilifon mwenye umri wa
miaka 16 aliyechukuliwa kijijini hapo tangu mwaka 2012 kwa lengo la
kwenda kufanya kazi za ndani mjini Arusha na kwamba baada ya ndugu
kukataa kupokea mwili askari polisi wamewakamata ndugu na mwaandishi wa
habari kwa madai kuwa wanahamasisha vurugu.
Kufatia
hali hiyo mkuu wa wilaya ya Muleba Bw. Lebris Kipuyo alilazimika kufika
eneo la vurugu na kuamuru askari polisi kutawanya wananchi ili magari
yaweze kupita na baadaye alifika hospitali na kuteuwa baadhi ya
ndugu,jamaa na wazazi wa mtoto ambao walikagua mwili wa marehem kisha
mkuu wa wilaya akawahutubia wananchi na kuwataka walioshuhudia mwili
waseme ukweli walichokiona nao bila kusita wamesema maiti inamajeraha
tumbo limetobolewa na sehemu za mwili zimekwaruzika kisha akavishwa nguo
na soksi ili kuficha ukweli.
Naye
mwaandishi wa habari wa kujitegemea gazeti la Mwananchi aliyejeruhiwa
na askari polisi kwa kupigwa virungu Bw. Shaban Ndyamkama amesema kuwa
yeye ndiye aliyetoa taarifa za vurugu hizo kwa mkuu wa wilaya ya Muleba
baada ya askari kufika eneo la tukio walimkamata na kumshambulia kwa
vipigo kisha wakamshikilia kwa muda hadi wananchi waliposhinikiza
kuachiwa kwake na baada ya waandishi wa ITV,Radio one kanda ya ziwa
kumuomba kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. George Mayunga ambaye
amekiri kwa njia ya simu kuwa vurugu hizo zimesababisha uvunjifu wa
amani na kumtaka mkuu wa polisi wilaya ya Muleba kumuachia huru
mwaandishi wa habari ambaye amepelekwa hospitali na wananchi kwa
matibabu zaidi.
chanzo:ITV