Ishu ilikuwa hivi, miaka
miwili iliyopita jijini Dar, Wastara alikuwa na wasanii wenzake kituoni
sasa daladala likapita karibu yao na kummwagia maji na alipojaribu
kumwambia kistaarabu kwamba hakufanya ‘fea’, dereva huyo akamuoneshea
ishara ya matusi.
Wastara uvumilivu ukamshinda, akamvaa
dereva huyo wa daladala na kumkwida ndipo vurugu kubwa ilipotokea maana
dereva huyo naye hakutaka kukubali, alianza kujibu mashambulizi kabla
wasanii waliokuwa na Wastara hawajamuamulia.
Alipotafutwa Wastara na kuulizwa juu ya kisa hicho, alicheka sana na kudai alikumbushwa mbali:“Hahahahahaha! Daah siku hiyo ilikuwa si mchezo alinimwagia maji tena yenye matope halafu namwambia ananitukana palikuwa hapatoshi kama tusingeamuliwa, angeipata.”