BEAUTIFUL Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25), amemlipua aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ‘K’ ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki.
Habari hiyo ya kuitwa mnafiki iliandikwa kwenye gazeti hili toleo lililopita iliyokuwa na kichwa kisemacho; ‘Kajala: Wema mnafiki’.
Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar, Wema alisema alishangaa kuona Kajala anamwita mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye tangu walipotofautiana kipindi cha nyuma kama alivyosema.
“Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie, itakuwa sahihi kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi? Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake? Nasema siyo sahihi kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye aliweka picha ya Dacutee na kumu-wish hajammaindi?” aliwaka Wema.
Akiendelea kutema cheche mbele ya kinasa sauti chetu, Wema alisema anachopaswa kuzungumza Kajala ni ukweli wa matatizo yao na siyo kusingizia watu wengine.
Akizungumzia ishu ya kukutana na Kajala na kupiga picha za pamoja wakiserebuka hivi karibuni, Wema alisema alifanya vile kuonesha kwamba hana kinyongo na ndiyo maana alivyoombwa apige picha na Kajala, hakusita kufanya hivyo.
“Mimi ni mtoto wa Kiislamu na nina imani na upendo kwa kila mtu, siwezi nikamkatisha mtu furaha yake na ndivyo ilivyotokea, niliombwa nipige picha ya pamoja na Kajala siku ile ya shughuli na nilifanya hivyo baada ya pale nikaenda zangu kulala,” alimalizia kusema Wema.
Bifu la mastaa hao wakali wa Bongo Movies liliibuka baada ya Wema kumtuhumu Kajala kuwa ametembea na aliyekuwa bwana’ke, kigogo aliyetajwa kwa jina la CK.