Gwiji: Mourinho (kushoto alimleta Drogba katika klabu ya Chelsea mwaka 2004 akitokea Marseille ya Ufaransa.
KLABU ya Chelsea inaangalia uwezekano wa kumrudisha Didier Drogba katika dimba la Stamford Bridge.
Nyota
huyo mwenye miaka 36 anazivutia klabu za Qatar, wakati Juventus nao
wakifikiria kumnasa mkongwe huyo anayecheza katika klabu ya Galatasaray
ya Uturuki.
Bado Jose Mourinho ana mahusiano mazuri na Muivory coast huyo na anavutiwa kumrudisha kwa majukumu ya ukocha zaidi.
Mkongwe huyu wa miaka 36 anazivutia klabu za Qatar, nao Juventus wanaitaka saini yake.
Klabu
hizo za Qatar zinatarajia kutoa ofa nono na mshahara utajadiliwa,
lakini unakadiriwa kuwa paundi milioni 3 kwa msimu baada ya makato ya
kodi.
Wazo la kurudi Chelsea litaangaliwa zaidi na pande zote.
Mourinho amekuwa na mapenzi makubwa kwa Drogba na anajua kuwa atakuwa na msaada mkubwa katika kikosi chake msimu ujao.
Alionesha
nia hiyo hata Galatasaray ilipokutana na Chelsea katika michuano ya
UEFA mwezi machi mwaka huu na alieleza kuwa Drogba anaweza kurudi na
yuko makini kufanikisha hilo.
Drogba
alishinda makombe matatu ya ligi, makombe manne ya FA na kombe la UEFA
akiwa katika klabu ya Chelsea na Mourinho anataka kutumia uzoefu wake
kuwashauri wachezaji wake wapya.
Drogba alikuwa shujaa wa Chelsea mwaka 2013 waliposhinda dhidi ya Bayern Munich na kutwaa ndoo ya UEFA