Trafiki akimdhibiti dereva wa gari dogo aina ya Toyota Pick
up.
SEKESEKE
la aina yake kati ya dereva wa gari dogo aina ya
Toyota Pick up na trafiki ambao majina yao hayakujulikana mara moja
liliibuka
na kuzua maswali mengi kwa mashuhuda huku mambo ya rushwa
yakitajwatajwa. Tukio hilo lilizozua maswali mengi liliibuka, Bamaga,
Mwenge jijini Dar jirani na kituo cha mafuta cha Bamaga.
Katika tukio hilo, dereva huyo na trafiki walikuwa
wakikunjana, ambapo dereva alikuwa akilalamika kuonewa (Haikujulikana kivipi)
wakati askari huyo wa usalama barabarani akisisitiza kuwa jamaa huyo alivunja
sheria.
Gari aina ya 'Land Rover' (break down) lililotumika kuvuta
gari la aina ya Toyota Pick up la dereva huyo.
ILIKUWAJE?
Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global
Publishers, kikiwa katika pitapita zake za kusaka matukio na kuhakikisha
maadili hayavunjwi ndipo kilipokutana na kisanga hicho cha kushangaza.
Trafiki alisikika akimwambia dereva kuwa amevunja sheria za
barabarani huku gari lake likiwa bovu hivyo aliamuru gari hilo kuvutwa hadi
kituoni kwa ajili ya ukaguzi lakini dereva huyo alikataa.
...ilikuwa ni vigumu sana kwa dereva huyo kukubali gari lake
kukamatwa.
DEREVA
Pamoja na kuelezwa kuwa gari lake lilikuwa na matatizo na
mahali alipoegesha hapakuwa sahihi, dereva huyo alipayuka: “Nawajua nyie
trafiki, kazi yenu ni kuonea watu sasa mimi sitoi kitu hapa, labda
mniue.“Siendi popote, mkiondoa gari nalala mbele yake ili mnigonge nife, mimi
nimesema silitoi.”
...dereva akizidi kubisha kwa uamuzi uliochukuliwa na afisa
usalama wa barabarani 'trafiki' .
TRAFIKI
Trafiki huyo aliyeonekana kuwa makini na kazi yake, hakuwa
na makuu, zaidi alitaka gari livutwe hadi kituoni huko sheria ingefuata mkondo
wake baada ya ukaguzi.
Mashuhuda wa tukio
hilo, waliliambia Ijumaa kuwa, kilichohitajika ilikuwa ni busara ya
masikilizano kuliko kuvutana kwa maneno na afisa wa polisi.
Afisa usalama wa barabarani akisisitiza kulichukua gari la
dereva huyo kwa ukaguzi zaidi.
“Sasa kama gari lake
anajua ni zima, anabishana nini na polisi? Ikiwa anajiamini kuwa aliegesha
sehemu sahihi, hofu yake ni nini? Kama kweli anajua yupo sawa, anatakiwa
kukubali kwenda polisi, gari likakaguliwe. “Wakati mwingine unaweza kuwalaumu
tu askari, kumbe ni tabia ya watu kukataa kutii sheria bila shuruti. Sasa
anafikiri kwa maneno makali anayotoa kwa huyo askari atamwachia?
Raia wakishuhudia mkasa huo uliotokea katika kituo cha
mabasi yaendayo Mwenge cha Bamaga.
“Anasema eti hatoi
kitu, kwani kaombw TWENZETa rushwa pale au anadhani kila trafiki anayemkamata
dereva aliyevunja sheria anataka rushwa?” alisikika shuhuda mmoja akihoji kwa
jazba.
Hata hivyo, pamoja na mkwara wa jamaa huyo, gari lake
lilifanikiwa kuvutwa kuelekea polisi ambapo jamaa huyo alipanda gari lingine
kulifuata.