MKUU wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Venance Mwamoto,
amevamia jukwaa la mkutano wa NCCR-Mageuzi na kisha kumtolea lugha ya matusi
Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali.
Mwamoto alijikaribisha kwenye mkutano huo uliokuwa
ukihutubiwa na Katibu Mkuu, Mosena Nyambambe kisha akaketi kiti cha mbele
walipokuwa viongozi wengine wa chama hicho na kuanza kumchokoza Mkosamali kwa
kumtolea
lugha chafu kwa sauti ya chini.
Mkuu huyo wa wilaya anadaiwa kufikia hatua hiyo ya
kuporomosha matusi kwa kilichoelezwa
kuwa alituhumiwa na Mkosamali kwenye
mkutano, kwamba amejimilikisha isivyo halali ekari 73 za ardhi katika Kijiji
cha Nduta wakati tayari anatumia wanajeshi kuwaondoa wanakijiji hao kwa kile
kilichodaiwa ni kutaka kubadili matumizi ya ardhi ili kijiji hicho kiwe
hifadhi.
Sokomoko hilo lilimalizwa kwa busara za wabunge, David
Kafulila (Kigoma Kusini) na Moses Machali (Kasulu Mjini) baada ya Mwamoto na
Mkosamali kukaribia kuzichapa kavu kavu jukwaani