Mwigizaji Irene Uwoya ambae alipata tuzo ya Steps kama mwigizaji bora kike 2012/2013 amethibitisha kuacha kuigiza movie kwa sasa ili kufanya kazi ambayo ameianza hivi karibuni.
Namkariri akisema: “Nimeamua kuacha mambo ya movie na kuwaachia wengine, haya maamuzi nimeyafanya kama miezi sita iliyopita. Mara ya mwisho kuigiza ni zaidi ya miezi sita iliyopita pia.”
Irene ambae ni mama wa mtoto mmoja kwa sasa anafanya show ya TV ya kusaidia Watanzania wanaoishi kwenye nyumba ambazo ni mbovu au hazina mahitaji muhimu yanayotakiwa kwenye nyumba.
Ni show ambayo haitahusika kujenga nyumba bali kuzirekebisha kwa gharama za mamilioni kwa kutegemea ubovu wa nyumba yenyewe, ambapo Irene amethibitisha hakuna kiwango cha mwisho cha pesa kama bajeti ya kutengeneza nyumba moja bali lengo ni kukarabati nyumba ikamilike.
Movie alizocheza mpaka sasa zinafika 40 lakini za kwake ni nne tu na amekiri kwamba kuacha kwake kuigiza hakuta mshushia kipato chake cha siku zote ambapo kwa movie moja ya kwake mwenyewe alikua anaiuza mpaka kwa milioni 35.
Show yake ya TV imeshaanza kuonekana Tanzania pamoja na kupata wadhamini ambao watamuwezesha kwenye kazi hii kubwa ya kupokea maombi ya Watanzania mbalimbali ambao wanahitaji nyumba zao zirekebishwe bure, kupitia kipindi hicho cha TV.