Rais Barack Obama.
Rais Barack Obama amelihutubia taifa Jumatatu usiku akisiistiza kwamba jeshi la taifa litaendelea na kazi zake wakati sehemu za
serikali kuu zinafungwa kuanzia leo Jumanne baada ya bunge kushindwa kukubaliana juu ya bajeti ya mwaka 2013 - 2014. Hatua hii inajulikana kama Government Shutdown.
serikali kuu zinafungwa kuanzia leo Jumanne baada ya bunge kushindwa kukubaliana juu ya bajeti ya mwaka 2013 - 2014. Hatua hii inajulikana kama Government Shutdown.
Baada ya wabunge wa Baraza la Wawakilishi kushindwa kukubaliana
ilipofika usiku wa manane Jumatau, juu ya bajeti ya matumizi, serikali
kuu ililazimika kutangaza kwamba sehemu za idara kadhaa zitabidi
kufungwa.
Mvutano wa kisiasa umekuwa ukiendelea bungeni kuhusiana na sheria ya
kihistoria ya Rais Obama, ya kutoa huduma nafuu za afya ambayo imekuwa
mashuhuri kwa jina la "Obamacare".
Baraza la wawakilishi linaoongozwa na chama cha Republican
liliidhinisha mswada wa matumizi ya serikali lakini kwa kuambatanisha
kufutwa kwa sheria ya Obamacare. Na mara tatu Baraza la Seneti
linalodhibitiwa na chama cha Demokrat limepinga mswada huo.
Kutokanana Bunge kutokubaliana juu ya kupitisha mswada wa kuongeza
muda wa matumizi ya serikali kuu sheria ya Marekani inahitaji idara zote
ambazo hazina shughuli muhimu kusita kufanya kazi kuanzia Oktoba mosi,
yaani leo Jumanne.
Jumla ya wafanyakazi wa serikali wapatao 800,000 wanakwenda likizo
bila malipo ambapo inatarajiwa kutakuwa na hasara ya dola bilioni moja
kwa wiki.
Chanzo: VOA