KELVIN YONDANI ATUA MJINI KAGERA KUIVAA KAGERA SUGER

Beki wa Yanga, Kelvin Yondani baada ya kutua mjini Bukoba, mkoani Kagera.
Na Mwandishi Wetu
BEKI Kelvin Yondani aliyeondolewa mazoezini na Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts, ametua mjini Bukoba na kikosi hicho, tayari kwa kuivaa Kagera Sugar, kesho.
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema hakuwa na ugomvi mkubwa na Yondani kama ilivyoelezwa na alichofanya ni kumuondoa mazoezini kwa kuwa hakujituma.
“Nani alisema kafukuzwa, sasa yuko hapa na sisi. Hakufanya juhudi nikamuondoa mazoezini, lazima watu wajifunze tofauti ya kufukuza na kuondoa.
“Ni kati ya wachezaji walio katika kikosi chetu na Jumamosi atacheza kama atakuwa katika hali nzuri,” alisema Brandts.
Kwa mujibu wa wenzake, leo Yondani ameonekana ni mwenye furaha tokea walipokuwa jijini Dar, Mwanza na baadaye mjini Bukoba ambako wana kibarua cha Ligi Kuu Bara, kesho dhidi ya Kagera.
Baada ya kuondolewa mazoezini kutokana na kutokimbia kwa kasi kama kocha alivyotaka, Yondani aliondoka zake.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...